Friday, July 4, 2014
KIKOSI MAALUM KUCHUNGUZA KIFO CHA BALOZI.
Do you like this story?
Siku
mbili baada ya Kaimu Balozi wa Libya, Ismail Nwairat kujiua kwa risasi akiwa
ofisini kwake, Jeshi la Polisi kupitia kikosi maalum cha uchunguzi wa matukio
ya kujiua, limeanza uchunguzi wa kifo hicho.
Akizungumza
jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema
watafanya uchunguzi wa kisayansi kwa kutumia maofisa maalum licha
ya taarifa za awali kuonyesha kuwa amejiua kwa risasi.
“Hatuchunguzi
kifo pekee kwa juu juu tu, hata kama imethibitishwa amejiua ni lazima
tuchunguze kwa nini amejiua, kwa mfano anaweza kuwa alitishiwa kuuawa au ana
matatizo ya kifamilia, ndiyo maana akajiua au mambo mengine,” amesema.
Alisema
ubalozi wa Libya umesharuhusu polisi kufanya uchunguzi ambao utashirikisha
kikosi maalumu na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambao watatoa ripoti ya
kidaktari ya uchunguzi wa kifo na maofisa wa ubalozi wenyewe.
“Ni
lazima tupate ruhusa ya kufanya uchunguzi kutoka Ubalozi wa Libya kwa sababu
kisheria masuala ya ubalozini ni ardhi ya Libya na polisi hawawezi kujichukulia
uamuzi hadi tupate baraka kwanza kutoka kwa ubalozi huo,”
Kova
alisema kuwa ripoti ya matokeo ya kifo hicho itatolewa baada ya muda mfupi
kwani polisi hawawezi kuchukua muda katika suala nyeti kama hilo la
mwanadiplomasia kujiua katika ardhi ya Tanzania.
ilisikika
hadi nje na kusababisha maafisa wa ubalozi kukimbilia kufahamu kulikoni.
Walipofika
walikuta mlango umefungwa kwa ndani, walivunja na kumkuta balozi akiwa katika
maumivu makali huku damu ikimminika kifuani,” amesema.
Kova
aliongeza kuwa maofisa hao walimpelekaa katika hospitali ya AMI Oysterbay
ambako alifariki dakika chache baadaye.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KIKOSI MAALUM KUCHUNGUZA KIFO CHA BALOZI.”
Post a Comment