Thursday, July 3, 2014
TFF,CRDB YATOA SEMINA KWA VIONGOZI WA MPIRA WA MIGUU MBEYA JUU MATUMIZI YA TIKETI ZA KIELEKTRONIKI.
Do you like this story?
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Nchini TFF pamoja na Benki ya CRDB wametoa mafunzo ya
matumizi ya tiketi za elektroniki mkoani Mbeya kwa kushirikisha
wasimamizi wa mechi katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine mbeya ,
viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya (MREFA).
Wengine
waliopatiwa mafunzo hayo , meneja wa Uwanja wa Sokoine na msaidizi wake,
makatibu wa Tanzania Prisons na Mbeya City, maofisa habari wa Mbeya City na
Tanzania Prisons, Ofisa Usalama wa MREFA na wasimamizi wa milangoni (stewards).
Semina hiyo
inalengo la kuwanda wadau hao katika kusimamia mfumohuo utakao anza
na timu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) za Mbeya City na Tanzania
Prisons kwa mchezo wao wa kirafiki Jumamosi (Julai 5 mwaka huu) kwenye Uwanja
wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Akizungumza
katika semina hiyo Ofisa wa mifumo ya kibenki ya kielektroniki,
Kalington Chahe, toka benki ya CRDB, mfumo huo unatoa fursa kwa kila mtu
kupata fursa ya kutazama mechi pasipo kuwa na usumbufu wa aina yoyote katika
hususani katika suala la ununuzi a tiketi.
Amesema kwa
kila mtu mwenye simu ya mkoni anauwezo wa kununua tiketi hata tano kwa wakati
mmoja na kuepuka suala la kulanguliwa na mawakala wasio waaminifu.
“Tumefanya
hivyo makusudi kwa kuwa tunaamini kuwa katika familia baba anaweza kununua
tiketi tano ambazo ataingia yeye na familia yake isiyozidi watu wane, hivyo
kufanya idadi ya watu kutoka familia moja kuwa watano” alifafanua Chahe.
Hata hivyo
amesema kuwa hali hiyo haizuii timu kununulia mashabiki wake tiketi za mchezo
kwani kutakuwa na utaratibu wake.
Akichangia mada
katika mafunzo hayo, mmoja wa washiriki , Charles Mwakipesile, alitoa
changamoto juu ya mfumo huo utakavyowezesha timu za majeshi zinazokuwa na
mashabiki wake maalumu ambao mara nyingi huingia bure uwanjani.
Mechi hiyo
ambayo itakuwa ya kwanza kuchezwa jijini Mbeya katika mfumo wa matumizi ya
tiketi za elektroniki kwa washabiki wanaoingia uwanjani itaanza saa 10 kamili
jioni.
Kiingilio
ni sh. 3,000 kwa majukwaa yote ambapo tiketi zimeanza kuuzwa leo (Julai Mosi
mwaka huu).
Wakati huo huo,
Afisa Habari wa TFF Boniface Wambura amesema kutakuwa na utaratibu
maalumu kwa waandishi wa habari za michezo kwa ajili ya kuripoti mechi hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TFF,CRDB YATOA SEMINA KWA VIONGOZI WA MPIRA WA MIGUU MBEYA JUU MATUMIZI YA TIKETI ZA KIELEKTRONIKI.”
Post a Comment