Thursday, July 3, 2014
MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AKUTANA NA MABALOZI WA OMAN NA SYRIA
Do you like this story?
Makamu wa Rais wa Jmahuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal leo Alhamisi Julai 03, 2014
amekutana na Waheshimiwa Mabalozi wa nchi za Oman na Syria wanaowakilisha nchi
zao hapa Tanzania. Mheshimiwa Makamu wa Rais amekutana na Mabalozi hao ofisini
kwake Ikulu jijini Dar es Salaam.
Awali alikuwa ni Balozi wa Oman,
Mheshimiwa Saoud Ali Mohammed Al-Ruqaish aliyefika kukutana na Mheshimiwa
Makamu na kufafanua kuwa uhusiano baina ya Tanzania na Oman unazidi kuimarika
na kwamba wawekezaji kutoka Oman wamekuwa wakija kwa wingi kuwekeza Tanzania
tofauti na siku za nyuma huku pia Tanzania ikionesha kufungua milango yake kwa
uwekezaji mkubwa wa kati nchini Tanzania.
Kwa upande wa Balozi wa Syria
Mheshimiwa Abdulmonem Annan yeye alimueleza Mheshimiwa Makamu wa Rais kuwa
Syria iko katika kipindi kigumu na kwamba nchi hiyo kwa sasa inatafuta kila
linalowezekana kurejesha amani. Balozi huyo alifafanua kuwa nchi yake inahitaji
msaada wa nchi za Kimataifa ili kusaidia kuweka pande zote zinazokinzana mezani
kwa lengo la kufikia maazimio yatakayoifanya nchi hiyo isiparanganyike.
Mheshimiwa Makamu wa Rais
alimueleza Balozi za Syria kuwa, Tanzania inatamani sana kuona hali ya utulivu
inarejea Syria na kwamba nchi hiyo inaendelea kujenga uchumi uliobomoka tayari.
Pia alisema kuwa msimamo wa Tanzania unabakia katika kutaka pande zinazohusika
katika mgogoro huo zinafuikia suluhu kwa amani ili wananchi wengi wasipoteze
maisha.
Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa
Rais
Ikulu Dar es Salaam
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AKUTANA NA MABALOZI WA OMAN NA SYRIA”
Post a Comment