Thursday, July 3, 2014
KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA MINJA AWATAKA WATANZANIA KUTHAMINI BIDHAA ZINAZOZALISHWA NA JESHI LA MAGEREZA
Do you like this story?
Watanzania wametakiwa kuthamini
na kutumia bidhaa zinazozalishwa na Jeshi la Magereza hapa nchini zikiwemo
Samani za ndani na Ofisi.
Mwito huo umetolewa na Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja wakati akiongea na
Waandishi wa Habari mara tu baada ya kutanganzwa rasmi Jeshi la Magereza kuwa
Mshindi wa kwanza kwa upande wa utengenezaji wa bidhaa za Samani za ndani
katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika uwanja wa
Mwalimu Nyerere uliopo Barabara ya Kilwa Wilayani Temeke, Jijini Dar es Salaam.
“Kuna Maboresho makubwa sana juu
ya utengenezaji wa bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na Jeshi la Magereza na
hiyo ndo imepelekea Jeshi la Magereza kuibuka Mshindi wa kwanza kwa upande wa
utengenezaji bora wa Samani za ndani katika Maonesho haya ya 38 ya Biashara yanayoendelea”.
Alisema Kamanda Jenerali Minja.
Aliwashukru Wananchi mbalimbali
kwa kuzipenda bidhaa zilizopo katika Banda la Jeshi la Magereza na kuwaomba
Wananchi kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya Mkoa wa DSM kutembelea
Banda la Jeshi la Magereza ili waweze kujipatia bidhaa bora pia kuona na
kujifunza.
Pia Kamishna Jenerali Minja
amewapongeza Maofisa na Askari wa Jeshi la Magereza wanaoshiriki katika
Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa kwa kufanikisha ushindi huo wa kwanza
kwa upande wa utengenezaji wa Samani za ndani katika Maonesho hayo
yanayoendelea, Jijini Dar es Salaam.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA MINJA AWATAKA WATANZANIA KUTHAMINI BIDHAA ZINAZOZALISHWA NA JESHI LA MAGEREZA”
Post a Comment