Thursday, July 3, 2014
MFARANSA SEAN GARNIER AJA TANZANIA KUONYESHA UMAHIRI WA KUCHEZA MPIRA WA MTAANI HUKU AKIBINUKA SARAKASI NA KUCHEZA DANSI
Do you like this story?
Mwanamichezo kutoka nchini
Ufaransa leo anatarajiwa kuonyesha shoo ya bure ambapo ataonesha umahiri wa kucheza
mpira wa mitaani, sarakasi na kucheza dansi.
Mfaransa huyo Sean Garnier ambaye
yuko nchini kwa ziara maalum ya kimichezo jana usiku alianza ziara hiyo kwa
kuonesha umahiri wake wa kucheza mpira wa mtaani katika viwanja vya ufukwe wa
Coco (Coco Beach) jijini Dar es Salaam.
Garnier ambaye anakipaji cha
kupiga danadana mpira huku akiweka mapozi mbalimbali alionekana kuwa kivutio
mbele ya mkutano na waandishi wa habari ambao walikuwepo kwenye mkutano huo
huku akionesha umahiri wake wa kupiga danadana na kucheza na mpira katika
barabara ya Alli Hassan Mwinyi baada ya mkutano huo.
Mwenyeji wa ziara ya Garnier,
Mkurugenzi wa Masoko Kampuni ya Mohan’s Vijay Joshi alisema kwamba huyu ni
mwanamichezo mwenye kushikilia taji la kipaji cha kucheza ‘Free Style’ duniani.
“Ameletwa kwa udhamini wa ‘Redbull
Street Sytle’ na atakuwa nchini kwa siku tano ambapo ni kati ya Julai 2 hadi
Julai 7 ataondoka.
Aidha mbali ya kumudu kucheza na
mpira pia nacheza sarakasi katika mitindo mbalimbali huku akiwataka watanzania
kuiga baadhi ya michezo ambayo ataionyesha akiwa atakapokuwa mtaani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MFARANSA SEAN GARNIER AJA TANZANIA KUONYESHA UMAHIRI WA KUCHEZA MPIRA WA MTAANI HUKU AKIBINUKA SARAKASI NA KUCHEZA DANSI ”
Post a Comment