Thursday, May 22, 2014
HAYA NDIYO MADHARA KWA WAJAWAZITO KULA UDONGO,WATOTO HUZALIWA MBUMBUMBU/ VILAZA DARASANI
Do you like this story?
Wanawake
wanaokula udongo wakiwa wajawazito wamo katika hatari ya kuwafanya watoto
watakowajifungua kutofanya vizuri shuleni.
Utafiti uliofanywa na shirika la African
Council for Gifted and Talented unaonyesha kuwa watoto ambao kina mama wao
walikuwa wakitumia udongo hawana akili darasani.
Mkuu wa shirika hilo Profesa
Humprey Obora amewaambia wanahabari jijini Nairobi kuwa utafiti huo umefanywa
kwa watoto wanaopelekwa katika taasisi hiyo ambayo hujihusisha kutambua na
kukuza vipawa vya watoto wakiwa bado wachanga.
Kwa kawaida wanawake wengi
hutumia udongo huo baadhi wakidai kuwa wana upungufu wa madini ila wengi wao
huzidisha matumizi yake.
Zaidi ya wazazi 4000 walihusishwa katika
utafiti huo lakini ni 1000 tu ambao maoni yao yalitumika kuandaa ripoti ya
utafiti huo.
Taasisi hiyo ilikuwa
ikifuatilia matokeo ya watoto hao wakiwa shuleni kwa muda wa miaka minne na
wakatambua kuwa wale ambao hawakuwa imara darasani mama zao walikuwa na historia
ya kutumia udongo wakiwa wamebeba mimba zao.
Watafiti hao wanasema kuwa
kutokana na hayo ubongo wa watoto waliozaliwa huchelewa kushika mambo.
Wasimamizi wa mradi huo
waliwahusisha wazazi kutoka katika sehemu mbalimbali nchini Kenya ambako kuna
vituo vya shirika la African Council for Gifted and Talented.
Kadhalika utafiti huo
unaonyesha kuwa wanawake katika miaka ya ishirini huwa na hamu kubwa kutumia
udongo.
via>>BBC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “HAYA NDIYO MADHARA KWA WAJAWAZITO KULA UDONGO,WATOTO HUZALIWA MBUMBUMBU/ VILAZA DARASANI ”
Post a Comment