Thursday, May 26, 2016
TAMISEMI YAZIAGIZA HALMASHAURI ZOTE KUKAMILISHA AGIZO LA MAGUFULI IFIKAPO MWEZI JUNI.
Do you like this story?
Na Daudi
Manongi- MAELEZO
HALMASHAURI
za Miji na Wilaya nchini zimekumbushwa kukamilisha zoezi la upatikanaji wa
madawati kwa shule za msingi na sekondari ifikapo juni 30 mwaka huu ili
kutekeleza agizo lililotolewa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Rai hiyo
imetolewa leo na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Rebecca Kwandu
wakati wa mahojiano na mwandishi wa habari hizi kuhusu uchakavu wa madarasa na
ukosefu wa madawati unaozikabili shule za kinesi A na B zilizopo wilaya ya
Rorya mkoani Mara.
“Suala
la upungufu wa madawati na uchakavu wa madarasa ni changamoto ya kitaifa na
kwamba lilishatolewa agizo na mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli kuhusu
halmashauri zote nchini kuhakikisha ifikapo Juni 30 mwaka huu kila mwanafunzi
anaketi kwenye Dawati” Alisema
Kwandu.
Kwa mujibu
wa Gwandu alisema Serikali ya awamu ya tano imepania kuinua kiwango na ubora wa
elimu nchini kupitia mikakati na sera ya elimu bure nchini kote.
Aliongeza
kuwa hatua hiyo imeibua changamoto kubwa kwa wanafunzi wengi kujitokeza kwa
asilimia kubwa na hivyo ni wajibu wa halmshauri hizo kukidhi mahitaji ya
madawati ili wasome katika mazingira mazuri.
“Mpaka
sasa Serikali imeendelea kutoa pesa kwa ajili ya elimu bure nchini kote na
kumekuwepo kwa changamoto mbalimbali kama upungufu wa walimu,madawati na
madarasa ambapo serikali inafanya jitihada za kila namna ili kutatua changamoto
hiyo”
Akifafanua
zaidi Gwandu alisema Serikali inaandaa harambee mbalimbali na kuongeza wigo wa
utoaji wa vibali vya kuchangia maendeleo ya elimu kwa hiari ili kutoa
nafasi kwa wadau mbalimbali wenye nia ya kufanya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TAMISEMI YAZIAGIZA HALMASHAURI ZOTE KUKAMILISHA AGIZO LA MAGUFULI IFIKAPO MWEZI JUNI.”
Post a Comment