Thursday, May 26, 2016
MAKANDARASI 4572 WAFUTIWA LESENI NCHINI
Do you like this story?
Bodi ya
Usajili wa Makandarasi imefuta usajili wa jumla ya makandarasi 4572 kwa
kushindwa kutimiza matakwa ya Sheria ya Usajili wa Makandarasi ya mwaka 1997.
Hayo
yamebainishwa na Kaimu Msajili wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB), Bw.
Rhoben Nkhori wakati wa Mkutano wa Mashauriano wa CRB uliofanyika jijini Dar es
Salaam na kufunguliwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
Bw. Nkhori
amesema kuwa katika jukumu la kuratibu mwenendo wa kazi za makandarasi, Bodi
ilikagua miradi 2735. Katika miradi hiyo iliyokaguliwa, miradi 1873 sawa na
asilimia 68.5 haikuwa na kasoro.
Ameongeza
kuwa miradi mingine ilikuwa na kasoro za kutofanywa na makandarasi
waliosajiliwa, kutozingatia usalama wa wafanyakazi, kutokuwa na bango wala uzio
na miradi kutosajiliwa. Kwa mujibu wa Bw. Nkhori miradi yote iliyopatikana na
upungufu wahusika walichukuliwa hatua mbali mbali kwa mujibu wa sheria.
Aidha,
Bwana Nkhori amesema kuwa kwa mwaka jana, Bodi ilisajili miradi 3,172 yenye
thamani ya shilingi trilioni4.23. Katika miradi hii asilimia 44.4 ilifanywa na
Makandarasi wazawa na asilimia 55.6 ilifanywa na makandarasi wa kigeni.
Licha ya
mafanikio hayo CRD ilikumbana changamoto kadhaa ikiwemo kuwasilisha nyaraka za
kugushi wakati wa usajili hususani kadi za magari na mitambo, vyeti vya wataalam,
kutumia majina ya makandarasi kwa udanganyifu kwa kuuza vibao, waendelezaji
kutotoa taarifa sahihi za umiliki kwa Bodi na baadhi ya makandarasi kushindwa
kuwalipa wafanyakazi na vifaa vya ujenzi.
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi, Bi Consolata Ngimbwa
amemwomba Mhe. Rais John Pombe Magufuli kuwapa kipaumbele Makandarasi wa humu
nchini ili kuwawezesha kiuchumi. “Mhe. Rais tunaomba utupe kipaumbele kwani
sisi tukipata hiyo miradi tutawekeza hapa nchi na kuongeza soko la ajira,”alisema
Bi Ngimbwa.
Katika
hotuba yake ya ufunguzi, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania amesema serikali yake itawapa kipaumbele makandarasi
wazawa lakini akawataka wajipange na kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia maadili
ikiwemo kujiepusha na vitendo vya rushwa.
Mkutano
huu pamoja na mamabo mengine utajadili jinsi ya kuwajengea uwezo makandarasi
nchini. Kauli mbiu ya Mkutano huo ni “Juhudi za Makusudi za kukuza uwezo wa
makandarasi wazawa, changamoto na mustakhabali.”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MAKANDARASI 4572 WAFUTIWA LESENI NCHINI”
Post a Comment