Thursday, May 26, 2016
MAKALLA AZINDUA MAANDALIZI YA NANENANE MBEYA.
Do you like this story?
NA
SAMWEL NDONI, MBEYA
MKUU wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla amesema kuwa Maonesho ya kilimo ya wakulima (Nane nane) kwa mwaka huu yatakuwa na tija kwa wakulima ili kuimarisha Sekta ya Kilimo nchini.
Akizungumza wakati wa kikao cha maandalizi ya sherehe za maonyesho (Nanenane) mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini,Makalla aliwataka wakuu wa Mikoa wa Kanda hiyo kuhakikisha Maonesho hayo yanawanufaisha wakulima.
Katika maandalizi hayo viongozi wa mikoa na wilaya kutoka kanda hiyo walikutana na kufanya kikao cha kwanza katika Ukumbi wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) uliopo ndani ya viwanja vya maonyesho ya nanenae vya John Mwakangale vya jijini Mbeya.
Makalla ambaye ni mwenyekiti wa vikao hivyo alisema karibia asilimia 80 ya mapato ya Halmashauri zote za mikoa ya ukanda huo yanategemea zaidi ushuru wa mazao hivyo akawataka kuboresha zaidi Sekta hiyo ili mapato yaendelee kuongezeka na hata kuimarisha hali ya chakula.
Makalla alisema kuwa kwa kiasi kikubwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini inazalisha mazao ya chakula kwa kiasi kikubwa hali inayofanya mikoa mingine kutegemea chakula kutoka katika mikoa hiyo, na hivyo akawataka kuongeza juhudi.
“Rais aliagiza kuwa mahali popote penye Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi, watu wanakufa njaa, viongozi hao watadhihirisha kuwa hawatoshi, hivyo ndugu zangu tunatakiwa kuhakikisha uzalishaji unaongezeka zaidi ili tuendelee kulisha mikoa mingine yenye uhaba wa chakula,” alisema.
“Lakini pia asilimia takribani 80 ya mapato ya Halmashauri zetu yanategemea zaidi ushuru wa mazao, hivyo kukutana kwa wakulima wetu kutasaidia kubadilishana teknolojia ya kilimo na kuimarisha mapato yetu,” alisema Makalla.
Awali akisoma taarifa ya maonyesho hayo, Katibu Tawala Msaidizi wa Uchumi na Uzalishaji wa Mkoa wa Mbeya, Nyasebwa Chimagu, alisema kuwa Kanda hiyo inatarajia kukusanya jumla ya shilingi milioni 141.8 kuanzia agosti mosi hadi agosti Nane.
Alisema kuwa mpaka kufikia mei 23 mwaka huu jumla ya wadau wa maonyesho 470 walikuwa wamepelekewa mialiko huku wadau 315 kati yao walikuwa wamethibitisha kushiriki na wanatarajia kuendelea kupokea watu wengine.
Hata hivyo alisema kuwa Mikoa itakayoshiriki katika maonyesho hayo zimeongezeka kutoka sita hadi saba huku Halmashauri zikiongezeka kutoka 32 hadi 40.
“Maonyesho ya mwaka uliopita tulikusanya kiasi cha shilingi milioni 96, lakini mwaka huu tunatarajia kukusanya kiasi cha shilingi milioni 141 kutokana na ongezeko la washiriki,” alisema Chimagu.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Steven Zerote, alitaka maonyesho hayo yawanufaishe zaidi wakulima kwa kuhakikisha wanafundishwa vya kutosha kilimo bora.
Alitaka zifanyike tafiti za kutosha kabla na baada ya maonyesho ili kujua mabadiliko yanayotokea.

Kauli mbiu ya Nanenane mwaka huu inasema ‘‘Kilimo, Mifugo, na Uvuvi ni nguzo ya Maendeleo, Vijana shiriki Kikamilifu ‘Hapa Kazi Tu’”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MAKALLA AZINDUA MAANDALIZI YA NANENANE MBEYA.”
Post a Comment