Tuesday, November 24, 2015

GUMZO!!! ETI MSHINDI WA TUZO ZA SURA MBAYA ZIMBABWE NI 'HANDSOME"


Mshindi namba moja wa shindano la mwanaume mwenye sura mbaya zaidi nchini Zimbabwe, Mison Sere.

Bingwa mtetezi mara tatu wa shindano hilo ambaye kwa sasa ametwaa nafasi ya pili, William Masvinu akiwa katika pozi.

Washiriki wote wa shindano hilo wakiwa jukwaa moja.  


Mison Sere akitabasamu wakati wa mashindano hayo.

Baadhi ya washiriki wa shindano hilo.  

Mison Sere na mkewe wakifufahia.


Harare, Zimbabwe
MJINI Harare nchini Zimbabwe, hivi karibuni kumefanyika mashindano ya kipekee ya kumpigia kura mwanaume mwenye sura mbaya zaidi katika taifa hilo, mashindano yaliyoitwa ‘MrUgly’.

Kama mashindano mengine ya urembo, shindano hili pia lilivutia washiriki wengi. Jopo la majaji lilikua na mengi ya kutahini kando na sura walitizama hulka na kujitanua kwa washindani

Kihoja kilizuka pale waamuzi walipomtaja Mison Sere, kuwa mshindi wa tuzo la mwaka huu la mtu mwenye sura mbaya zaidi nchini Zimbabwe akimbwaga mpinzani wake ambaye ni bingwa mtetezi wa tuzo hizo William Masvinu akiambulia nafasi ya pili.

Hata hivyo mashabiki wa bingwa mtetezi huyo, Masvinu walilalamikia uamuzi huo wakidai kuwa Mison Sere alikuwa na sura nzuri tu ‘handsome’ licha ya mwanya mkubwa na tabasamu kama ya kibogoyo.

Licha ya majibizano makali Sere mwenye umri wa miaka 42, alipewa tuzo hiyo na kuzawadiwa pesa kiasi cha dola $500, sawa na shilingi 1,000,000 za Kitanzania.

Yeye na mke wake walishangilia tuzo hilo jukwaani na kuwatonesha kidonda wafuasi wa mpinzani wake waliowazomea na hata kuzua vurugu wakidai kapendelewa.
‘Walihoji umauzi wa majaji wakisema kuwa hakuwa na sura mbaya ila alikuwa kang’oa meno yake ya mbele ili atwae ushindi huo.’

”Hayo sio maumbile ya kutisha, kukosa meno?
”Inakuwaje wanampuuza bingwa wa zamani William Masvinu ambaye maumbile yake yanatisha mno”, walisikika mashabiki wa Masvinu. Mwisho wa mjadala huo ulibakia vivyo hivyo.

Bingwa mara tatu wa tuzo za mtu mwenye sura mbaya zaidi nchini Zimbabwe William Masvinu alikwenda nyumbani akiwa na mfadhaikom mkubwa baada ya kuikosa nafasi ya kwanza.

‘Huyu bwana hatishi kamwe, hebu tazama pua langu kubwa uso wangu mweusi na unavyotisha, sikio langu ni kama la popo ni kubwa itakuwaje kuwa amenishinda?’
‘La sikubaliani na uamuzi huu wa leo, nimeudhika sana.” Masvinu alisikika akinung’unika.

0 Responses to “GUMZO!!! ETI MSHINDI WA TUZO ZA SURA MBAYA ZIMBABWE NI 'HANDSOME"”

Post a Comment

More to Read