Tuesday, November 24, 2015
MGOGORO WA ZANZIBAR WATUA IKULU YA MAREKANI
Do you like this story?
Na Swahilivilla, Washington
Wakati
vikao vya siri vya kutafuta suluhu ya mzozo wa kisiasa visiwani Zanzibar vikiwa
vimeripotiwa, juhudi za kuupatia ufumbuzi mzozo huo zimehamia kutoka Ikulu ya
Zanzibar na kufika Ikulu ya Marekani (White House).
Mnamo tarehe 21 mwezi huu, Wazanzibari waishio nchini
Marekani waliandamana hadi kwenye Ikulu ya nchi hiyo katika juhudi za kutafuta
uingiliaji kati wa kimataifa ili kuupatia suluhisho mzozo huo.
Akizungumza
na waandishi wa habari mbele ya Ikulu hiyo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Wazanzibari Waishio nchni Marekani (ZADIA) iliyoandaa maandamano hayo Bwana
Omar Haji Ali, alisema kuwa maandamano hayo yanakuja katika juhudi za Jumuiya
hiyo za kutafuta uingiliaji kati wa kimataifa katika kuukwamua mgando wa
kisisas visiwani Zanzibar.
Aliendelea kusema kwamba maandamno hayo pia yana lengo la
kumkumbusha rais Barack Obama wa Marekani kutekeleza ahadi yake ya kuilinda
demokrasia Barani Afrika.
"Katika
hotuba yake aliyoitoa kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Afrika mapema mwaka huu,
rais Obama alisema '.. pale ambapo raia hawawezi kutekeleza haki zao, basi
ulimwengu una jukumu la kukemea. Na Marekani itafanya hivyo, hata kama wakati
mwingine itakuwa inauma'..", alikumbusha
Bwana Ali.
Aliongeza kuwa "Wananchi wa Zanzibar
wameshindwa kutekeleza haki yao kwa zaidi ya nusu karne sasa. Wakati umefika
sasa kwa ulimwengu kuchukua jukumu lake. Wakati umefika sasa kwa Marekani siyo
tu kukemea, lakini pia kuchukua hatua za kivitendo ili kuhakikisha kuwa sauti
za Wazanzibari zinasikilizwa na kuheshimiwa"
Alipoulizwa
ni hatua gani watakazochukuwa iwapo Serikali ya Marekani haikuchukua hatua yoyote
kusaidia kumaliza mgando wa kisiasa Zanzibar, Bwana Ali alisema;
"Tuna imani na rais Obama, na tumemfikishia barua ya malalamiko yetu, na tunasubiri jibu lake, na imani yetu ni kuwa atachukua hatua madhubuti khususan ikizingatiwa kuwa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ulikuwa wa mwanzo kutoa taarifa kuelezea kuwa uchaguzi wa Zanzibar ulikuwa wa haki na huru"
Alidokeza kuwa, iwapo hali itaendelea kubakia kama ilivyo, basi ZADIA itaelekea kwenye Umoja wa Mataifa.
"Tuna imani na rais Obama, na tumemfikishia barua ya malalamiko yetu, na tunasubiri jibu lake, na imani yetu ni kuwa atachukua hatua madhubuti khususan ikizingatiwa kuwa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ulikuwa wa mwanzo kutoa taarifa kuelezea kuwa uchaguzi wa Zanzibar ulikuwa wa haki na huru"
Alidokeza kuwa, iwapo hali itaendelea kubakia kama ilivyo, basi ZADIA itaelekea kwenye Umoja wa Mataifa.
Katika maandamano hayo yaliyowashirikisha pia wapenda amani
na demokrasia kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni, waandamanaji walibeba
mabango yaliyokuwa na maneno kama vile "Mshindi wa uchaguzi
atangazwe", "maamuzi ya Wazanzibari yaheshimiwe", "bila
haki hakuna amani' na mengineyo.
Aidha, waandamanaji hao walipiga makelele wakidai
"tunataka matokeo yetu ya uchaguzi.."
Akizungumza
na Swahilivilla, raia mmoja wa Marekani aliyeshiriki kwenye maandamano hayo
alisema "Nilimpeleka mwanangu kwenda kusoma kule, bado ana mapenzi
na Zanzibar, na amenisimulia habari nzuri za amani, utulivu na ukarimu wa watu
wake. Amekuwa akifuatilia hali ilivyo, na kwa hamasa kubwa alipopata habari za
maandamano haya, akaniomba tuje kuwaunga mkono Wazanzibari katika kudai haki
yao"
Itakumbukwa kuwa, wananchi wa Zanzibar walipiga kura mnamo
tarehe 25 Oktoba mwaka huu, lakini Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar
(ZEC) Bwana Jecha Salum Jecha akatangaza kufutwa kwa uchaguzi huo Mkuu visiwani
humo, kitendo ambacho wataalamu wa Sheria wamesema kuwa kinakwenda kinyume na
Katiba ya Zanzibar.
Wachambuzi wanaona kuwa hatua hiyo ya Bwana Jecha ilikuja
wakati asilimia kubwa ya matokeo yaliyokuwa yametangazwa yalikuwa yanampa
ushindi mgombea wa urais wa Zanzibar kutoka chama cha upinzani cha Wananchi
(CUF) Maliim Seif Shariff Hamad.
Kitendo cha kufutwa kwa uchaguzi huo ambao wachunguzi wa nje
na ndani waliulezea kuwa ulikuwa wa haki na huru, kimezua mtafaruku wa kisiasa
visiwani Zanzibar, na juhudi za ndani na nje zimekuwa zikifanyika ili kumaliza
mgogoro wa kisiasa visiwani humo.
Maandamano ya ZADIA ni katika juhudi za hivi karibuni kabisa za kimataifa za kusaka suluhu za mgogoro huo kwa njia za amani.
Maandamano ya ZADIA ni katika juhudi za hivi karibuni kabisa za kimataifa za kusaka suluhu za mgogoro huo kwa njia za amani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MGOGORO WA ZANZIBAR WATUA IKULU YA MAREKANI”
Post a Comment