Thursday, May 26, 2016
RAIS MAGUFULI AKEMEA VITENDO VYA RUSHWA KWA WAKANDARASI WAZAWA ......AWATAKA WATANGULIZE MASLAHI YA TAIFA
Do you like this story?
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka wakandarasi
kote nchini kufanya kazi kwa kutanguliza maslai ya taifa, badala ya kutaka
kupata faida kubwa kupita kiasi kutoka kwenye zabuni za miradi ya ujenzi
wanayopata kutoka serikalini.
Dkt.
Magufuli amesema hayo leo tarehe 26 Mei, 2016 alipokuwa akifungua mkutano wa
mashauriano wa bodi ya usajili wa wakandarasi kwa mwaka 2016 unaofanyika kwa
siku mbili katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es salaam.
Rais Magufuli
amesema serikali yake ipo tayari kuwapa kipaumbele wakandarasi wa Tanzania pale
inapotangaza zabuni za miradi ya ujenzi, lakini amewataka kujirekebisha kwa
kupanga viwango vinavyostahili vya gharama za ujenzi wa miradi hiyo ambavyo
serikali itaridhika.
“Nawatolea
mfano, idara ya mahakama imetangaza kujenga mahakama za mwanzo na za wilaya,
kwenye bajeti wana shilingi bilioni 24, makadirio ya kitaalamu yanaonesha kila
jengo lisizidi shilingi milioni 200, wakandarasi wazalendo walipoomba katika
nyaraka zao wametaka jengo moja lijengwwe kwa shilingi bilioni 1 na milioni
400, sasa nakuuliza Mheshimiwa Mwenyekiti na ndugu wakandarasi, hata kama una
upendeleo, upendeleo huo utapasua moyo.
“Hata
kama utakuwa na upendeleo kiasi gani kwa wazalendo utashindwa, sasa mimi
niwaombe ndugu zangu wakandarasi, pamoja na nia nzuri ya serikali kuwasaidia
wakandarasi wazalendo ni lazima na ninyi muwe na nia nzuri ya kuisadia nchi” Amesema Rais Magufuli
Pamoja na
hilo, Rais Magufuli ametaka wakandarasi hao kuacha kutoa rushwa kwa watendaji
wa serikali pale wanapoomba zabuni za ujenzi na badala yake amewataka kutoa
taarifa kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (TAKUKURU) ili watendaji hao
wakamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria.
“Mimi
niwaombe wakandarasi, msikubali kutoa rushwa, na muwafichue watendaji wanaoomba
rushwa, atakapokuomba wewe rushwa hujui amewaomba wangapi, na utakapotoa rushwa
huna hakika kama ile tenda utaipata, wengine wameishia kutoa rushwa hapa,
rushwa hapa, rushwa hapa mpaka anafilisika, kazi huipati na rushwa umeitoa” Amesisitiza Dkt. Magufuli.
Aidha,
Rais Magufuli ametoa wito kwa wakandarasi hao kujipanga ipasavyo ili waweze
kupata zabuni katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya ujenzi itakayofanywa hapa
nchini ikiwemo ujenzi wa bomba la mafuta la kutoka Hoima nchini Uganda hadi
Bandari ya Tanga hapa Tanzania, Ujenzi wa Reli ya Kati na Ujenzi wa Viwanda.
“Sina
uhakika kwamba mmejipangaje wakandarasi wa Tanzania katika kuhakikisha hiyo
kazi mnaipata ya kujenga bomba kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga.
“Nitasikitika
sana kilometa zote 1,410 pasiwepo mkandarasi hata mmoja wa kutoka Tanzania,
wenzetu wanajipanga, na ninavyoona wakandarasi wa Tanzania wameendelea sana,
lakini nashindwa kuelewa kuna tatizo gani linatufanya kutojua changamoto
zinazotukabili, tumejipanga kujenga reli ya kati (Standard Gauge) kwenye bajeti
ya mwaka huu tunaanza na kilometa 100, lakini kuna fedha nyingine zitatolewa na
serikali ya China, tutajenga zaidi ya kilometa 1,200 (Standard Gauge, Central
Corridor) itakayounganisha Mwanza, Kigoma, Burundi na Rwanda. Wakandarasi wa
Tanzania mmejipangaje? " ameuliza
Rais Magufuli.
Mkutano
huo pia umehudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa TAKUKURU Kamishna Valentino Mlowola ambaye amesema Taasisi hiyo ipo
tayari kukabiliana na rushwa iliyopo katika sekta ya ujenzi ambayo ni miongoni
mwa sekta zenye rushwa kubwa na ametaka wakandarasi watoe ushirikiano kukomesha
tatizo hilo.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es
salaam
26 Mei,
2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ RAIS MAGUFULI AKEMEA VITENDO VYA RUSHWA KWA WAKANDARASI WAZAWA ......AWATAKA WATANGULIZE MASLAHI YA TAIFA”
Post a Comment