Thursday, July 3, 2014
SIRI YAFICHUKA KUHUSU KUCHAKAA SANA KWA NOTI YA SHILINGI 500.
Do you like this story?
BENKI Kuu ya
Tanzania (BoT) imesema sababu ya noti ya sh. 500 kuchakaa mapema ni
kutokana na kutumika na watu wengi wasio na mzunguko wa huduma za kibenki.
Akizungumza
katika Maonesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba), Ofisa
wa BoT, Abdul Dollah, alisema noti zote zinatengenezwa kwa malighafi ya aina
moja, lakini kinachotokea ni noti ya sh. 500 kutumika kupita kiasi.
"Ni asilimia 14 ya Watanzania
ndio wanatumia huduma za kibenki, waliosalia hawatumii, sasa ukija katika noti
za sh. 500 na 1,000, zinachoka sana maana ndizo zinazoshikwa na watu wengi wa
tabaka la kawaida"
amesema.
Aliwataka wale
wenye noti zilichokaa kuzirudisha BoT, ili wapatiwe noti mpya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SIRI YAFICHUKA KUHUSU KUCHAKAA SANA KWA NOTI YA SHILINGI 500.”
Post a Comment