Thursday, July 3, 2014
UNAAMBIWA KWA MARA YA KWANZA TANZANIA IMETENGENEZA BOTI ISIYOTUMIA NAHODHA!
Do you like this story?
Mamlaka ya
Mafunzo na Ufundi Stadi (Veta) imevumbua boti inayojiendesha bila nahodha
ambayo ina uwezo wa kutuma taarifa za kijasusi na kujilinda dhidi ya
mashambulizi au uharibifu unaoweza kufanywa na watu wenye nia mbaya.
Akizungumza wakati
wa Maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) katika
Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini hapa jana, Mvumbuzi wa mashine hiyo,
Immanuel Bukuku alisema kuwa imemchukua miezi sita kufanikisha uundaji wa
mashine hiyo.
Alisema
uvumbuzi huo umeambatana na majaribio ambayo yamefanyika katika Pwani ya
Kigamboni na yameonyesha mafanikio makubwa na ipo tayari kwa ajili ya matumizi
ikiwa na kamera za kutosha kwa ajili ya uchunguzi na kupeleka taarifa.
Uvumbuzi umekamilika na boti
ipo tayari kwa ajili ya matumizi na wadau wanakaribishwa kwa ajili ya kusaidia
ufanikishaji wa utengenezaji wa boti nyingine zaidi
alisema na
kuongeza kuwa boti hiyo itakuwa inaongozwa na mashine nyingine itakayo kuwa
sehemu maalumu.
Bukuku ambaye
ni mwalimu wa masuala ya Sayansi na Teknolojia katika Chuo cha Veta Chang’ombe
alisema amevumbua boti hiyo ambayo imetengenezwa kwa kutumia vifaa rafiki na
mazingira ya bahari na inatumia mfumo wa umeme jua na mashine za kuzalisha
umeme.
Ina uwezo wa kuhisi kuwapo kwa
mtu au chombo kingine jirani yake na kutoa taarifa katika sehemu ambako
kinaratibiwa, pia ina uwezo wa kushambulia kwa kutumia mitutu na ina uwezo
mkubwa katika masuala ya ulinzi na usalama
alisema.
Alisema pia
amefanikiwa kutengeneza injini ya ndege ambayo imeonyesha mafanikio kwa kiasi
kikubwa na wakati wowote inaweza kutumika na mafanikio hayo yanachangiwa kwa
kiasi kikubwa na mpango wa Veta wa kuwa na Kitengo cha Masuala ya Ufundi na
Ubunifu.
Kuna mashine na teknolojia
nyingi ambazo zimevumbuliwa hapa, ni dalili njema na tuna matumaini kuwa
uvumbuzi zaidi unafuata kutokana na tafiti nyingi kuonyesha dalili za mafanikio
alisema na
kuongeza kuwa kitengo hicho kimepania kubadili mwelekeo mzima wa Veta kwa hivi
sasa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “UNAAMBIWA KWA MARA YA KWANZA TANZANIA IMETENGENEZA BOTI ISIYOTUMIA NAHODHA!”
Post a Comment