Thursday, July 17, 2014
TIDO MHANDO "KUONDOKA" GAZETI LA MWANANCHI.
Do you like this story?
Na Mwandishi
wa MCL, Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Tido Mhando
amewaaga wafanyakazi wa kampuni hiyo baada ya kumaliza mkataba wake wa miaka
miwili na nusu.
Mkataba wa
Tido katika kampuni ya Mwananchi utafika kikomo mwishoni mwa mwezi huu.
Taarifa ya
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Nation Media Group (NMG), Linus Gitahi kwa wafanyakazi
wote wa Afrika Mashariki ambako kampuni hiyo inamiliki vyombo vya habari,
inasema Mhando anaondoka MCL huku akiacha mafanikio makubwa katika nyanja zote
na kwamba atakumbukwa kwa mchango wake.
MCL ni
kampuni tanzu ya NMG inayochapiSha magazeti ya Mwananchi, Mwananchi Jumamosi,
Mwananchi Jumapili, The Citizen, The Citizen on Saturday, Sunday Citizen na
Mwanaspoti.
Kabla ya kuwa
Mkurugenzi Mtendaji wa MCL mwaka 2012, Mhando alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa
Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kati ya mwaka 2006 na 2010. Awali alikuwa
Mkuu wa Idara ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la BBC (1999-2006).
Mhando
aliiwezesha MCL kukua kwa kasi kubwa katika mapato na katika mpango wa
uchapishaji wa magazeti ya MCL Kanda ya Ziwa ambako wakazi wa mikoa hiyo sasa
wamekuwa wakisoma magazeti asubuhi tofauti na zamani.
Wafanyakazi
wa MCL walimpongeza kwa kuboresha masilahi yao kwa kipindi cha uongozi wake na
kuandaa misingi bora ya uongozi, ikiwamo kumwandaa mrithi wake.
Akiwaaga
wafanyakazi jana asubuhi, Mhando aliwashukuru kwa ushirikiano wao pia alisema
amejifunza mambo mengi mapya, ikizingatiwa kuwa kwa miaka mingi alikuwa kwenye
sekta ya habari ya utangazaji tofauti na uchapishaji. “Safari hii ilinipa
uzoefu mpya na wenye changamoto nyingi lakini kupitia ushirikiano wenu wa dhati
tulifanikiwa kuiweka kampuni katika hali nzuri,” alisema Mhando.
Gitahi
alisema nafasi ya Mhando itachukuliwa na aliyekuwa Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa
MCL (COO), Francis Nanai.
Nanai
alijiunga MCL , Agosti mwaka jana akitokea Kampuni ya Saruji ya Mbeya Cement
(Lafarge Tanzania) ya mkoani Mbeya akiwa Mkurugenzi wa Biashara.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TIDO MHANDO "KUONDOKA" GAZETI LA MWANANCHI.”
Post a Comment