Friday, September 25, 2015
MAHUJAJI WANNE WATANZANIA WAFARIKI, MAKKA.
Do you like this story?
Miili ya mahujaji walikufa kwenye tukio hilo ikiwa imefunikwa. |
Muonekano wa umati wa mahujaji katika mji wa Makka. |
Makka, Saudi Arabia
MAHUJAJI wane Watanzania
wamethibitishwa kufariki dunia katika tukio la kukanyagana lililotokea jana
huko Mina katika mji wa mtakatifu wa Makka nchini saudi Arabia.
Watanzania hao waliopoteza maisha ni miongoni
mwa mahujaji 717 kutoka sehemu mbalimbali za dunia waliopoteza maisha na
wengine zaidi ya 800 katika tukio hilo wakati wa siku ya mwisho ya Hija (jana).
Taarifa ya Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Abu
Bakari Zuberi iliyotolewa akiwa Makka imewataja watanzania watatu waliokwisha
tambulika majina yao kuwa ni Bi. Mwanaisha Hassan Juma, Mkungwe Suleiman Hemedi
na Sefu Saidi Kitimla.
Mtanzania mwingine mwanamke aliyekufa jina
lake bado halijatambulika, pia yupo raia mmoja wa Kenya Bi. Fatuma Mohammed
Jama ambaye alisafiri Makka kwa kutumia wakala wa Tanzania.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MAHUJAJI WANNE WATANZANIA WAFARIKI, MAKKA.”
Post a Comment