Friday, September 25, 2015

RAIS WA CUBA ZIARANI MAREKANI


Rais wa Cuba Raul Castro


Rais wa Cuba amewasili mjini New York, ikiwa ni mara ya kwanza kuwasili nchini Marekani katika kipindi cha miaka 15 iliyopita.

Rais Raul Castro yuko nchini humo kwa ajili ya kushiriki mkutano wa Baraza la Umoja wa Mataifa utakaofanyika wiki ijayo.

Afisa mmoja wa serikali ya Cuba, Prensa Latina amesema Rais Castro pia leo anaweza kusikiliza hotuba ya kiongozi wa kanisa katoliki atakayoitoa katika Umoja wa Mataifa, ambaye alisaidia kuchangamsha mahusiano kati ya nchi hizo mbili.

Rais Castro pia anatarajiwa kuhudhuria mkutano wa umoja wa Mataifa kuhusu Malengo endelevu ya Maendeleo, mwishoni mwa wiki.BBC

0 Responses to “RAIS WA CUBA ZIARANI MAREKANI”

Post a Comment

More to Read