Wednesday, May 3, 2017
VPL JUMAMOSI ZIPO 5, YANGA-PRISONS, JUMAPILI SIMBA-LYON!
Do you like this story?
Kwa
mujibu wa Kanuni ya 5 ya michuano ya ASFC kuhusu Uwanja wa mashindano
inasema: “Uwanja wa mashindano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports HD
utakuwa ni uwanja wenye hadhi inayokubalika na TFF.”
LIGI KUU YA VODACOM BARA KUENDELEA JUMAMOSI, JUMAPILI
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, inatarajiwa kuendelea Jumamosi Mei 6 na Jumapili Mei 7, mwaka huu kwa jumla ya michezo sita.
Kwa mujjibu wa ratiba, michezo ya Jumamosi kutakuwa na michezo mitano ilihali Jumapili kutakuwa na mechi moja.
Michezo
ya Jumamosi itakuwa ni kati ya Toto African na JKT Ruvu Uwanja wa CCM
Kirumba jijini Mwanza wakati Majimaji ya Songea itakuwa mwenyeji wa
Mwadui kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma.
Kagera
Sugar itaalikwa na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko
Mlandizi mkoani Pwani wakati Young Africans ya Dar es Salaam itaialika
Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Siku
hiyo ya Jumamosi Mei 6, mwaka huu Azam FC itaialika Mbao FC ya Mwanza
kwenye Uwanja wa Azam Complex ulioko Mbagala, Dar es Salaam ilihali
Jumapili kutakuwa na mchezo kati ya Simba SC na African Lyon kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wakati mechi zote zitaanza saa 10.00 jioni, mchezo kati ya Azam na Mbao utaanza saa 1.00 usiku.
SERENGETI BOYS YAPANGIWA LIBREVILLE
Timu
ya Tanzania ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 maarufu kwa jina
la Serengeti Boys, imebadilishiwa kituo kutoka Port Gentil na sasa
imepangiwa Libreville.
Serengeti
Boys imepangwa kundi B pamoja na timu za Niger, Angola na Mali ambako
watafungua nayo mchezo Mei 15, mwaka huu. Kwa mabadiliko hayo, Kundi A
lenye timu za Cameroon, Ghana, Guinea pamoja na wenyeji Gabon, litakuwa
Port Gentil.
Kwa
sasa Serengeti Boys wako Cameroon kwa kambi ya wiki moja iliyoanza
Aprili 29, mwaka huu ambako tayari imecheza na wenyeji Cameroon mchezo
mmoja na kushinda bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa
uliofanyika jijini Yauonde.
Wenyeji
hao, Cameroon watarudiana na Serengeti Boys katika mchezo mwingine wa
kirafiki wa kimataifa utakaofanyika kesho Jumatano, Mei 3, mwaka huu.
…………………………………………………………………………….
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “VPL JUMAMOSI ZIPO 5, YANGA-PRISONS, JUMAPILI SIMBA-LYON!”
Post a Comment