Wednesday, May 3, 2017
UEFA CHAMPIONZ LIGI: RONALDO HATARI, AIFYEKA ATLETICO 3 KWENYE EL DERBI MADRILENO HUKO BERNABEU!
Do you like this story?
UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI
Nusu Fainali – Mechi za Kwanza
Jumanne Mei 2
Real Madrid 3 Atletico Madrid 0
++++++++++++++++
JANA
huko Estadio Santiago Bernabéu Jijini Madrid Nchini Spain Mechi ya
Kwanza ya Nusu Fainali ya Kwanza ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, kati ya
Mahasimu wakuu wa Mji huo Real Madrid na Atletico Madrid ambayo
hubatizwa El Derbi Madrileno, ilichezwa na Mchezaji Bora Duniani
Cristiano Ronaldo aliibuka Shujaa kwa kubamiza Bao zote 3 wakati Real
ikishinda 3-0.
Hii
ilikuwa ni mara ya 5 kwa Timu hizi kupambana katika Mechi za Ulaya na
Real Madrid walimaliza ndoto za Atlético Madrid kwenye UCL katika Misimu
Mitatu iliyopita, ikiwa ni pamoja wa Fainali za Mwaka 2014 na 2016, na
safari hii hali inaelekea ni hiyohiyo labda Atletico wamudu kubadilika
katika Marudiano Wiki ijayo wakiwa kwao Vicente Calderon na kupindua
kipigo hiki cha 3-0.
Ronaldo
aliipa Real Bao lao la Kwanza Dakika ya 10 kwa Kichwa alipounganisha
Krosi ya Casemiro na kupiga Bao nyingine 2 Dakika za 73 na 86.
Hii
ni mara ya Pili mfululizo kwa Ronaldo kupiga Hetitriki kwani katika
Mechi 2 zilizopita za Robo Fainali za UCL dhidi ya Bayern Munich alipiga
Hetitriki kwenye Mechi hizo alizofunga Jumla ya Bao 5.
Ronaldo ndie Mfungaji Bora katika Historia ya UCL akiwa na Bao 103.
Hii Leo ipo Mechi nyingine ya Kwanza ya Nusu Fainali ya UCL huko Monaco kati ya AS Monaco na Juventus.
VIKOSI:
REAL MADRID: Navas, Carvajal, Ramos, Varane, Marcelo, Kroos, Casemiro, Modrić, Isco, Benzema, Ronaldo
REAL MADRID: Navas, Carvajal, Ramos, Varane, Marcelo, Kroos, Casemiro, Modrić, Isco, Benzema, Ronaldo
Akiba: Casilla, Nacho, James Rodríguez, Kovačić, Vázquez, Asensio, Morata
ATLÉTICO MADRID: Oblak, Lucas Hernández, Savić, Godin, Filipe Luis, Koke, Gabi, Saúl Ñíguez, Carrasco, Griezmann, Gameiro
ATLÉTICO MADRID: Oblak, Lucas Hernández, Savić, Godin, Filipe Luis, Koke, Gabi, Saúl Ñíguez, Carrasco, Griezmann, Gameiro
Akiba: Moyà, Tiago, Torres, Correa, Thomas, Gaitán, Alberto Rodríguez
REFA: Martin Atkinson [England]
UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI
Nusu Fainali – Mechi za Kwanza
**Mechi kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku, Saa za Bongo
Jumatano Mei 3
AS Monaco v Juventus
TAREHE MUHIMU:
MECHI ZA MTOANO:
02–03/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Kwanza
09–10/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Pili
03/06/17: Fainali (National Stadium of Wales, Cardiff)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ UEFA CHAMPIONZ LIGI: RONALDO HATARI, AIFYEKA ATLETICO 3 KWENYE EL DERBI MADRILENO HUKO BERNABEU! ”
Post a Comment