Tuesday, May 2, 2017
AUDIO: ‘Ni vizuri matetemeko madogomadogo yaendelee kutokea’ -RC Kagera
Do you like this story?
Kufuatia tetemeko llililotokea
kwa mara nyingine mkoani kagera majira ya saa 7 na dakika 29 za usiku wa
kuamkia April 30 mwaka huu,mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jeneral Mstaafu Salum Kijuu amesema kuwa tetemeko hilo lilikuwa na ukubwa 3.1 vipimo vya ritchel.
‘Wanasema
lile tetemeko lilitokea ziwani eneo la Minziro, zile ni after shocks za
lile lililotokea mwaka jana mwezi wa tisa na wanasema ni vizuri
yaendelee kutokea hayo madogomadogo kuipa nafasi miamba ipumue kuliko
kukaa muda mrefu miaka na miaka alafu linatokea kama lile la mwaka
jana’–RC Kijuu
‘Wanasema hizi after shocks
zitakuwepo na zitaendelea kuwepo ni miamba inapumua,muhimu tuzingatie
yale tuliyokuwa tunashauliwa na wataalamu mbalimbali wa miamba waliokuja
na tuachane na taaruki‘-RC Kijuu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “AUDIO: ‘Ni vizuri matetemeko madogomadogo yaendelee kutokea’ -RC Kagera”
Post a Comment