Monday, May 1, 2017

TIMU YA VIONGOZI WA SERIKALI MBEYA YAIBAMIZA TIMU YA VIONGOZI WA DINI MABAO 4 KWA 1


Kiongozi wa Timu ya Serikali Mh Amosi Makalla (kushoto)akimsalimia kiongozi wa Timu ya Dini Mh David Mwashilindi Meya wa Jiji la Mbeya kabla ya Mpambano huo.




Goli kipa wa Timu ya Serikali Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Dhahiri Kidavashari akiingia kwa madoido uwanjani.





Picha ya pamoja timu ya Serikali mara baada ya kuchukua kombe.


Viongozi wa.serikali mkoa wa.Mbeya wamewakimbiza viongozi wa dini katika mchuano wa kombe la Amani kwa kuwacharaza magoli 4-1.

Mchuano huo ulioisindikiza siku ya Mei Dei ulitawaliwa na burudani ya kipekee katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Washindi Serikali ya Mkoa walitawazwa kwa kukabidhiwa Kombe la Amani lililopokelewa na Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla
Burudani pekee katika mchuano huo ilikuwa ni golikipa wa timu ya serikali RPC Kidavadhari.

0 Responses to “TIMU YA VIONGOZI WA SERIKALI MBEYA YAIBAMIZA TIMU YA VIONGOZI WA DINI MABAO 4 KWA 1”

Post a Comment

More to Read