Wednesday, May 3, 2017
UCL-NUSU FAINALI: HISTORIA IPO KWA JUVE ILA MONACO WANAE TINEJA KYLIAN MBAPPE!
Do you like this story?
NUSU
FAINALI ya Pili ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, itachezwa Jumatano Usiku
Stade Louis II, Monaco kati ya Wenyeji AS Monaco na Juventus ya Italy.
Mechi
hii inakutanisha Difensi imara dhidi ya Washambuliaji hatari huku
Monaco wakisifika kwa kupiga Bao nyingi wakati Juve wakifungwa Goli
chache.
Monaco ni Timu yenye Vijana wengi wakati Juve ina Wakongwe na Wazoefu wengi.
Wakati Juve wakitumia Mfumo wa 4-2-3-1 chini ya Kocha Max Allegri ambao huhakikisha Pjanic, Dybala, Higuain, Mandzukic pamoja na Maveterani Buffon,
Chiellini, Bonucci na Dani Alves wote kuwepo Uwanjani, Monaco, chini ya
Kocha kutoka Ureno Leonardo Jardim, wao hung'ara kwa Mfumo wa kasi wa
4-4-2 unaotoa mwanya kwa Tineja wao wa Miaka 18 Kylian Mbappe kuliza
Watu.
Tineja
huyo, ambae amefunga Bao 18 katika Mechi 18 zilizopita, hupata sapoti
kubwa toka kwa Almamy Toure, Bejamin Mendy, Bernardo Silva, na Nabil
Dirar huku Radamel Falcao akiibuka upya Msimu huu na kupiga Bao 28.
Hii
ni mara ya kwanza kwa Monaco kutinga Nusu Fainali tangu 2004 lakini
mara 2 wamepigwa na Juventus kwenye Mashindano haya ya Ulaya.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
Juventus (Mfumo 4-2-3-1): Buffon, Dani Alves, Bonucci, Chiellini, Alex Sandro, Pjanic, Marchisio, Cuadrado, Dybala, Mandzukic, Higuain
Monaco (Mfumo 4-4-2): Subasic, Dirar, Glik, Fabinho, Toure, Silva, Moutinho, Bakayoko, Lemar, Mbappe, Falcao
REFA: Antonio Mateu Lahoz (Spain)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “UCL-NUSU FAINALI: HISTORIA IPO KWA JUVE ILA MONACO WANAE TINEJA KYLIAN MBAPPE!”
Post a Comment