Monday, August 18, 2014
JUMA MWAMBUSI SASA AANZA MAJIGAMBO KUELEKEA LIGI KUU BARA.
Do you like this story?
SIKU chache baada ya timu yake kuanza
ziara katika mikoa jirani na Mbeya, Kocha wa Mbeya City, Juma Mwambusi ametamba
timu yake itafanya maajabu ambayo yatashangaza wadau wengi wa soka nchini
tofauti na msimu uliopita.
Mwambusi alisema ana mbinu mpya kabisa
atakazozitumia kwa vijana wake huku akiwataka wapenzi na mashabiki wa timu hiyo
kutegemea mambo makubwa msimu ujao.
Kocha huyo alitoa kauli hiyo juzi
Jumamosi mjini Sumbawanga alipokuwa akizungumzia malengo na mikakati yake ya
msimu ujao wa Ligi Kuu ya Bara wakati timu hiyo ikifanya ziara ya kuwatembelea
mashabiki na wapenzi wake mikoa ya Rukwa na Katavi ikiwa ni maandalizi ya
kuingia rasmi kambini.
Akizungumza na Mwanaspoti, Mwambusi
alisema: “Mipango yangu ni kuiona Mbeya City inatwaa ubingwa, msimu uliopita
tulikuwa na hofu ya ugeni kwenye ligi hiyo lakini tulifanya vizuri. Msimu huu
Mbeya City inakuja kivingine kabisa wapenzi na mashabiki wetu wategemee mambo
makubwa msimu ujao.
“Baada ya kupata mialiko kutoka kwa
mashabiki wetu walioko Rukwa na Katavi ya kuwatembelea nimeona ni fursa nzuri
ya kucheza mechi za kirafiki na wenyeji ili kuweza kuangalia kasoro zilizopo
kwa wachezaji wangu kwani wametoka mapumzikoni.”
Katika msimu uliopita Mbeya City
iliyoshiriki ligi kuu kwa mara ya kwanza, ilimaliza katika nafasi ya tatu huku
ikitoa changamoto kubwa kwa timu zilizoshiriki ligi hiyo.
Chanzo:Mwanaspoti
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “JUMA MWAMBUSI SASA AANZA MAJIGAMBO KUELEKEA LIGI KUU BARA.”
Post a Comment