Thursday, August 7, 2014

KESI NZITO YAFUNGULIWA TENA DHIDI YA MICHAEL JACKSON, MLALAMIKAJI ATOA USHAHIDI WA KULAWITIWA UTOTONI.



Michael Safechuk na Michael Jackson wakiwa London, 1988


Wakati Michael Jackson akiwa amelala kwenye nyumba yake ya milele, bado familia yake imeendelea kuandamwa na tuhuma nzito zinazomhusu mfalme huyo wa Pop duniani.
Mlalamikaji, James Safechuck mwenye umri wa miaka 36 hivi sasa ambaye alikuwa katika kesi ya Michael Jackson ya mwaka 2005 kuhusu ulawiti, ameibuka tena na kufungua kesi na kutoa ushahidi mpya wa jinsi alivyokuwa akilawitiwa na marehemu mwaka 1988 wakati akiwa mtoto mwenye umri wa miaka 10 tu.
James ambaye sasa ni baba wa familia hakuonesha ushirikiano wakati wa kesi ya mwaka 2005 licha ya kutajwa kama sehemu ya ushahidi.
TMZ wameeleza kuwa wamepata nyaraka zilizowasilishwa na Safechuck mahakamani ambazo zinaeleza kuwa Michael Jackson alimfundisha lugha ya ishara wakati akiwa na umri wa miaka kumi, lugha ambayo alikuwa akiitumia kutaka kumueleza kuwa anataka kufanya nae mapenzi.
Ameeleza kuwa moja kati ya ishara hizo ni pale walipokuwa wakishikana mikono kusalimiana, alikuwa anambinya au kumtekenya katikati ya kiganja.
Katika nyaraka hizo ameendelea kueleza kuwa MJ alikuwa anamchukua na kumpeleka kwenye majumba ikiwa ni pamoja na sehemu inayoitwa ‘The Hideout’ ambapo walikuwa wakinywa vinywaji laini, pink wine na kuangalia video za ngono.
Amesema marehemu aliendelea kumfanyia vitendo hivyo  hadi pale alipoanza kubalehe.
Hata hivyo, mwanasheria wa Michael Jackson, Howard Weitzman ameiambia TMZ kuwa kesi hiyo inatakiwa kutupiliwa mbali kwa kuwa imeletwa kwa mara ya kwanza miaka 20 baada ya tukio hilo analolieza na kwamba James Safechuck aliwahi kula kiapo na kueleza kuwa Michael Jackson hakumfanyia kitu chochote kibaya.

0 Responses to “KESI NZITO YAFUNGULIWA TENA DHIDI YA MICHAEL JACKSON, MLALAMIKAJI ATOA USHAHIDI WA KULAWITIWA UTOTONI.”

Post a Comment

More to Read