Friday, August 8, 2014
KOMBE LA KAGAME KUTIMUA VUMBI LEO, AZAM FC KUTUPA KARATA YA KWANZA NA RAYON.
Do you like this story?
MICHUANO ya Kombe la Kagame inaanza
kutimua vumbi leo hii Agost 8 hadi 24 mwaka huu mjini Kigali nchini
Rwanda, ambapo timu 14 zitawania taji
linaloshikiliwa na mabingwa watetezi, Vital’O ya Burundi.
Wawakilishi wawili wa Tanzania katika
michuano hiyo, KMKM ya visiwani Zanzibar na mabingwa Tanzania wa ligi kuu soka
Tanzania bara, Azam fc watashuka dimbani leo katika mechi za ufunguzi.
KMKM watacheza mechi ya ufunguzi ya
kundi A dhidi Altabara ya Sudan kusini katika uwanja wa Nyamirambo.
Wana Lambalamba, Azam fc waliopo kundi
moja A timu hiyo ya Zanzibar, watajitupa
uwanjani jioni kuoneshana ufundi na wenyeji Rayon Sport katika dimba la taifa,
Amahoro mjini Kigali.
Azam fc waliokwenda Kigali na kikosi
kamili gado wanatazamiwa kutoa upinzani mkubwa wa Rayon ambao watakuwa na faida
kubwa ya mashabiki.
Baada ya mechi ya Azam, usiku katika
dimba hilo hilo, mchezo mmoja wa kundi B utachezwa baina ya timu ya zamani ya
kocha wa Simba sc, Zdrvako Logarusic na KCCA ya Uganda.
Kesho Agosti 9 mwaka huu katika dimba
la Amahoro mechi mbili za kundi C na
moja ya kundi B zitapigwa.
Mapema itaanza mechi ya mabingwa
Vital’O ya Burundi dhidi ya Benadir ya Somalia ikifuatiwa na mechi ya jioni
baina ya Police ya Rwanda na El Merreikh ya Sudan.
Baadaye usiku maafande wa jeshi, APR ya
Rwanda watachuana na Flambeau ya Burundi.
Azam fc watashuka dimbani tena Agosti
10 mchana kuchuana na KMKM ya Zanzibar, mchezo wa kundi A.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KOMBE LA KAGAME KUTIMUA VUMBI LEO, AZAM FC KUTUPA KARATA YA KWANZA NA RAYON.”
Post a Comment