Friday, August 22, 2014
MFANYAKAZI WA HOSPITALI YA PERAMIHO SONGEA AJINYONGA
Do you like this story?
Mwili wa Fredrick Mgaya (60) ukiwa unaning’inia katika mti aliojinyongea , Tunaomba radhi kwa picha hii. |
Songea Mwanaume mmoja Fredrick Mgaya (60), mkazi wa Peramiho,
Songea mkoani Ruvuma amejinyonga usiku wa kuamkia leo katika maeneo yaliyo
karibu na viwanja vya michezo vya Abasia kijijini Peramiho.Mwanaume huyo
aliyekuwa akifanya kazi kitengo cha maabara katika Hospitali ya Peramiho na
kustaafu mnamo mwezi aprili mwaka huu amekutwa amejinyonga majira ya asubuhi ya
leo. Marehemu Fredrick Mgaya amekutwa na ujumbe katika mfuko wa shati
lake, ulioelezea chanzo kilichopelekea yeye kujitoa uhai. Afande Allen
Urio ambaye alikuwa mmoja wa mashuhuda wa kwanza,anasema “ Nilikuwa natoka
lindo asubuhi ndipo nikakuta kundi la wanafunzi wa shule ya msingi wakiwa
njiani, nikawauliza kwanini wamesimama badala ya kwenda shule muda ule, ndipo
waliponiambia kuna mtu ananing’inia kwenye mti pale.
Nilipofika kwenye mti huu ndipo nilipomkuta mzee wetu Fredrick Mgaya
akiwa ameshapoteza maisha.
Ni tukio la kusikitisha sana kwani ni mzee wetu katika jamii ambaye
tulikuwa tunaishi naye vizuri. Mbali na migogoro yake na mkewe lakini uamuzi
aliouchukuwa unasikitisha na si mzuri kabisa.
Kama mlinda amani katika jamii napenda kuwaasa wananchi wajaribu kutafuta
suluhu ya matatizo kwa namna nyingine na sio kwa kujitoa uhai”
Akiongea Hakimu wa mahakama ya mwanzo kijijini Peramiho bi Maria
Sambo amesema, ameshaletewa na kusuluhisha migogoro ya ndoa hiyo ya marehemu
mara mbili na hadi sasa kuna kesi inayoendelea katika mahakama ya Hakimu mkazi,
lakini kwa hali ya kawaida hakudhani kwamba marehemu Fredrick Mgaya
angefikia hatua hiyo ya kujitoa uhai.
Nao mashuhuda wa tukio hilo wakiongea kwa masikitiko, wengi wamelaani
uamuzi uliofikiwa na mzee Mgaya kwani ni dhahiri alikuwa ni mtu wa watu na pia
alikuwa ni tegemeo la familia yake ambayo amewaacha ghafla.
Uamuzi ambao umesababisha maumivu kwa wanajamii hususan ndugu, jamaa
pamoja na marafiki wengi waliokuwa wakimpenda na kushirikiana naye kwa mambo
mengi ya kimaisha.
Mwenyekiti wa kijiji cha Peramiho A Bwana Joseph Ngonyani ameonesha
masikitiko yake ya dhati kwa kuondokewa na moja ya wazee aliokuwa akiwategemea
kwa ushauri katika kijiji chake.
“Tukio hili linagusa sana unajua, kwasababu linahusu mtu wa karibu
sana na ambaye tunashinda nae siku zote bila kujua nini kinamsibu na nini
anakipanga katika akili yake”.
Ndoa nyingi sana zinasumbuliwa na migogoro ya hapa na pale, hivyo ni
vizuri watu wa ustawi wa jamii na asasi zinazohusiana na jamii kujaribu kutoa
mafunzo na maelekezo ya jinsi ya kutatua migogoro hiyo ili kuepusha adha kama
hii isijitokeze tena ndani ya jamii yetu.
Alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo bwana Ignasi Kapinga.
Winfried Thadei Mgaya, mdogo wa marehemu anasema, amepokea tukio
hilo kwa mshtuko na kwa majonzi sana. Anapata uchungu sana juu ya msiba wa kaka
yake kwani marehemu ameacha watoto wanne ambao bado ni tegemezi pamoja na
mjane. Pia amesema mazishi yatafanyika tarehe 7 jumamosi kijijini kwao
Madaba, Songea mkoani Ruvuma.Habari kwa hisani ya Demashonews
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MFANYAKAZI WA HOSPITALI YA PERAMIHO SONGEA AJINYONGA”
Post a Comment