Saturday, August 16, 2014
RAIS WA COLOMBIA AUNGA MKONO MATUMIZI YA BANGI.
Do you like this story?
![]() |
Rais wa Colombian Juan Manuel Santos |
![]() |
Bhangi inakuzwa kwa wingi nchini Colombia |
Rais wa Colombian Juan Manuel Santos amesema kuwa anaunga mkono matumizi ya bangi kwa minajili ya utabibu.
Bwana Santos ameunga mkono mswada ambao utapigiwa kura bungeni wakati wowote kwa manufaa ya kupunguza uchungu kwa wagonjwa.
Rais huyo amesema kuwa kuhalalishwa kwa Bangi kutawanyima
walanguzi wa mihadarati biashara kwani itakuwa sio haramu kupatikana na bangi
nchini humo.
Colombia ni moja kati ya mataifa ambayo yamekumbwa na vita vya walanguzi wa madawa ya kulevya na serikali vita ambavyo vimesababisha mauaji ya mamia ya watu. .
Marijuana inakuzwa kwa wingi nchini Colombia, lakini taifa hilo linajulikana kote duniani kwa ukuaji wa cocaine, kwa pamoja na Peru.

Asilimia kubwa ya madawa hayo kulingana na takwimu yanauzwa
nchini Marekani ambapo yanaingizwa kisirisiri kupitia mataifa ya Marekani ya
kati na Mexico.
"natumai tutaliangazia jambo hili la matumizi ya marijuana kwa mtazamo mpya utakaofaidi wagonjwa ambao wanaitegemea kupunguza uchungu.'' alisema Santos akiwa mjini Bogota.BBC
"natumai tutaliangazia jambo hili la matumizi ya marijuana kwa mtazamo mpya utakaofaidi wagonjwa ambao wanaitegemea kupunguza uchungu.'' alisema Santos akiwa mjini Bogota.BBC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ RAIS WA COLOMBIA AUNGA MKONO MATUMIZI YA BANGI. ”
Post a Comment