Thursday, August 21, 2014
RASIMU YA WARIOBA YACHANWA CHANWA.
Do you like this story?
Kuna kila dalili kwamba mabadiliko mengi
yaliyopendekezwa katika Rasimu ya Katiba yakigusa miundo ya taasisi nyeti za
umma yatawekwa kando na huenda Bunge Maalumu likatoa Katiba isiyokuwa na
mabadiliko makubwa kama ilivyotarajiwa.
Gazeti
hili limebaini kuwa kamati nyingi za Bunge hilo zimebadili mapendekezo mengi
hasa yanayowagusa viongozi na taasisi nyeti kama Bunge, tofauti na
ilivyopendekezwa katika Rasimu ya Katiba iliyoandaliwa na Tume ya Mabadiliko ya
Katiba chini ya uongozi wa Jaji Joseph Warioba.
Miongoni
mwa mambo ambayo yamependekezwa kurejeshwa kama yalivyokuwa ni muundo wa Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambalo kwa mujibu taarifa kutoka kwenye
kamati mbalimbali, ni kuendelea na muundo wa sasa unaowajumuisha wabunge kutoka
Zanzibar.
Katika
maelezo yake, Jaji Warioba alisema moja ya kero za muungano katika eneo la
Bunge ni malalamiko kwamba wabunge kutoka Zanzibar wamekuwa wakishiriki katika
Bunge la Muungano na kushiriki kujadili mambo yanayohusu Tanzania Bara.
Kupitia
mfumo wa Serikali tatu, Rasimu ilikuwa na mapendekezo ya kuwapo kwa Bunge la
Muungano lenye wabunge 75, lakini mapendekezo hayo pia yamefutwa katika kamati
karibu zote na kurejesha mfumo wa sasa pamoja na uwapo wa Baraza la Wawakilishi
la Zanzibar.
Mwenyekiti
wa Kamati Namba Tano, Hamad Rashid Mohamed alisema jana kuwa suala la muundo wa
Bunge lilisababisha mvutano mkubwa katika kamati yake na baadhi ya wajumbe
walikuwa wakihoji uwakilishi mkubwa wa wabunge wa Zanzibar katika Bunge la
Muungano hata kwa mambo ya Tanzania Bara.
Hata
hivyo, alitetea hali hiyo akisema uwapo wa wabunge kutoka Zanzibar ni moja ya
masharti yaliyowekwa na Katiba. “Hata Katiba ya sasa imeweka sharti la idadi ya
wabunge wa Zanzibar, hilo nalo ni sharti la Katiba huwezi kuliondoa, kama
unataka kuliondoa unapotunga Katiba maana yake ni lazima uvunje muungano.”
Alisema
mwaka 1964 mambo yote ya Tanganyika yaliingizwa kwenye Serikali ya Muungano...
“Kwa hiyo ni lazima ukafumue Muungano, useme haya ni ya Tanganyika na haya ni
ya Muungano,” alisema.
Hamad
alisema katika hadidu ya rejea, Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilikatazwa kugusa
mambo ya Muungano. “Hivi wabunge 70 wanaokuja kutoka Zanzibar wakazungumzia
mambo ya Bara, hivi kuna dhambi gani, sioni kosa kabisa.” Mwenyekiti huyo
alisema kamati yake imebaini kwamba Rasimu ya Warioba ina upungufu mwingi kwani
hata baadhi ya kero zilizotajwa zilishafanyiwa kazi na Serikali.
Hoja
ya ushiriki wa Wazanzibari katika masuala ya Tanzania Bara iliripotiwa kuibuka
katika Kamati Namba Moja ambako mmoja wa wajumbe, Ally Keissy alinikuliwa
akihoji sababu za wajumbe wa Zanzibar kushiriki mambo ambayo wao siyo sehemu
yake.
Via >Mwananchi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “RASIMU YA WARIOBA YACHANWA CHANWA.”
Post a Comment