Monday, August 25, 2014
SEHEMU YA BARABARA YA MANDELA JIJINI DAR KUFUNGWA LEO
Do you like this story?
Mkandarasi mkuu anaeshughulikia
mradi wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam, Strabag International
ametangaza kufungwa kwa muda kipande cha barabara ya Mandela hadi makutano ya
Ubungo Mataa kuanzia leo.
Akiongea jana na waandishi wa
habari, Ofisa Uhusiano wa kampuni hiyo, Bw. Yahya Mkumba alisema kipande cha
barabara ya Mandela kuanzia makutano ya barabara ya morogoro upande wa kushoto
uelekeo wa Tabata kuanzia ubungo mataa hadi darajani patafungwa.
Kipande hicho kitafungwa kuanzia
tarehe 25/08/2014 mpaka tarehe 30/08/2014 ili kupisha ujenzi wa kipande cha
barabara hiyo na hivyo kuwalazimu watumiaji wa barabara hiyo kutumia barabara
ya upande mmoja.
Akifafanua zaidi ofisa uhusiano
huyo alisema magari yatakayokuwa yanatokea Mwenge, Kimara na Shekilango
yatalazimika kutumia barabara ya upande wa kulia ambayo pia itakuwa ikitumika
na magari yanayo toka Tabata kuelekea Ubungo.
“Tunaomba radhi kwa usumbufu
utakaotokea,” alisema Bw. Mkumba.
Mradi wa Mabasi yaendayo haraka
unatarajiwa kuondoa adha ya foleni katika jiji hilo na kuleta ufanisi wa
usafiri.
Awamu ya kwanza ya mradi huo
inatarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwaka huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SEHEMU YA BARABARA YA MANDELA JIJINI DAR KUFUNGWA LEO”
Post a Comment