Friday, September 12, 2014
SITTA AWAPA SOMO VIONGOZI WA UKAWA.
Do you like this story?
Na Benedict Liwenga, MAELEZO-Dodoma.
MWENYEKITI wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta amewaadaa baadhi
ya viongozi wanaojiita UKAWA kwa taarifa yao ya kutaka kumfikisha Mahakama ya
Uhalifu wa Kimataifa kwa kuendeleza mchakato huo wa Katiba.
Kauli hiyo
imetolewa leo 12 Septemba, 2014 mjini Dodoma na Mhe. Sitta kufuatia baadhi ya
viongozi hao, kudai kuwa watampeleka katika mahakama hiyo.
Mhe. Sitta
ameeleza kuwa baadhi ya viongozi wa kundi hilo kuwa wanakipaji kikubwa cha
uigizaji huku akifafanua kuwa wakati walipokuwa Bungeni wakati wa mchakato wa
kupiga kura za siri, viongozi wa kundi hilo walizifanya kura hizo kuwa wazi na
baadaye kuja na kauli kuwa Bunge Maalum la Katiba linaloendelea sasa sio halali
lihairishwe.
“Juzi Mhe.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amekutana nao mara mbili kwa muda wa saa Saba
na katika kukutana huko wakafikia maafikiano, lakini siku moja baadaye wao
wamekana yote waliyokubaliana hapa mjini Dodoma, kwa hiyo ni vyema wananchi
wakawapima hawa watu”, alisema Mhe. Sitta.
Aidha, Mhe. Sitta aliasa kwa kusema kuwa wananchi na viongozi wanatakiwa
kujua kuwa mchakato wa bunge Maalum la Katiba sio jambo la mzaha na wao hawapo
hapo bungeni kwa mzaha mzaha.
“Mimi nawaambia kuwa hapo mwakani watakaposhindwa uchaguzi basi warejee
katika fani zao ambazo Mwenyezi Mungu kawajalia”, alisema Mhe. Sitta.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)


0 Responses to “SITTA AWAPA SOMO VIONGOZI WA UKAWA.”
Post a Comment