Friday, June 27, 2014
SERIKALI YAPIGA MARUFUKU TRAFIKI KUYAVIZIA MAGARI VICHAKANI NA KUYASIMAMISHA GHAFLA.
Do you like this story?
Serikali
imepiga marufuku tabia ya askari Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani,
kuvizia magari katika barabara kuu wakiwa na kifaa cha kupima mwendo kasi wa
magari.
Naibu Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Peraira Silima, alisema tabia hiyo ya trafiki ni kinyume
cha sheria na zinaweza kusababisha ajali.
Hata hivyo,
Silima aliwataka madereva kutii Sheria za Barabarani ikiwemo kupunguza
mwendokasi na kufafanua kuwa, wakati mwingine askari hutafuta kivuli na hatua
hiyo isichukuliwe kuwa wanavizia magari.
Katika swali
lake, Ngoye alitaka Serikali ieleze ni hatua gani zimekuwa zikichukuliwa
kuhakikisha madereva wanafuata sheria zilizowekwa kama inavyofanyika katika
nchi nyingine.
Ngoye pia
alitaka Serikali ieleze kwa nini madereva wameendelea kutumia magogo, mawe na
majani yenye miba barabarani kuashiria kuwa kuna gari limeharibika, na
wakiondoka wanayaacha na wengine wameendelea kuendesha magari huku wakisikiliza
simu.
Naye Mbunge
wa Musoma Mjini, Vincent Nyerere (Chadema), alihoji kama ni sahihi kwa trafiki
kuvizia magari na kifaa cha kupima mwendo kasi.
Akifafanua
majibu ya maswali hayo, Silima alisema trafiki kujificha na chombo hicho na
kujitokeza kusimamisha gari ni kinyume cha sheria kwa kuwa tabia
hiyo inaweza kusababisha ajali.
Kuhusu
matumizi ya magogo, majani na mawe, alisema ni kinyume na Sheria na kutaka
madereva watumie alama za pembe tatu ambazo ni nzito na kuachana na alama hizo
ambazo ni nyepesi ambazo hupeperushwa na upepo.
Silima pia
alionya kuwa Serikali iko mbioni kuanza kuwanyang’anya leseni za udereva
madereva wote ambao watathibitika kukithiri kwa makosa ya usalama barabarani,
na kuzuiwa kabisa kufanya kazi hiyo.
Hatua hiyo
itaanza kuchukuliwa mara baada ya kukamilika na kuanza kwa Mfumo mpya wa Nukta,
ambao utaweka kumbukumbu za makosa ya madereva ambayo itatumika kuwachukulia
hatua hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ SERIKALI YAPIGA MARUFUKU TRAFIKI KUYAVIZIA MAGARI VICHAKANI NA KUYASIMAMISHA GHAFLA.”
Post a Comment