Sunday, April 5, 2015
MAITI YENYE UTATA YAFUKULIWA NA KUKUTWA IMEKATWA SEHEMU YA VIUNGO NA SEHEMU ZA SIRI.
Do you like this story?
Hali ya taharuki imewapata wakazi wa kijiji cha Park Nyigoti
kata ya ikoma wilaya ya Serengeti baada ya mahakama kutoa ruhusa ya kufukuliwa
kwa mwili wa Bi. Celina Jumapili aliyefariki dunia na kuzikwa tarehe tatu Machi
kisha kuonekana utata katika kaburi lake.
Kufuatia hali hiyo leo kaburi lake limefukuliwa na kukuta
sehemu ya viungo vya mwili wake vimekatwa vikiwemo kiganja cha mguu
vidole vya mkono wa kushoto na sehemu za siri zikiwa zimenyofolewa hali
iliyozua mashaka makubwa kwa wakazi wa kijiji hicho.
Mwandishi wa habari hzi alifika katika kijiji cha Park
Nyigoti wilayani Serengeti na kushuhudia zoezi la kufukua kaburi likiendelea
ambapo inadaiwa kuwa marehemu Celina alifariki dunia tarehe mbili ya Machi na
kuzikwa tarehe tatu lakini tarehe ishirini na mbili ndugu walikuta sehemu ndogo
ya kaburi likiwa limefukuliwa.
Hali hiyo ndiyo ikawafanya wananchi wakataka kuhakiki kuwa
mwili wa ndugu yao upo au umechukuliwa na baada ya kupata kibali cha
mahakama wamefukua na kukuta viungo hivyo vikiwa vimekatwa na watu wasio
julikana.
Akielezea namna tukio ilo lilivyo tokea mama wa marehemu
Celina Bi Nyahende Kwihamba amesema tukio hilo limewaweka katika mashaka
makubwa kutokana na kijiji hicho kushamiri kwa tabia ya ushirikina na kuiomba
serikali isaidie kumaliza tabia hiyo.
Kijiji cha Park Nyigiti mara kwa mara kimekuwa na matukio ya
kikatili kwani tarehe mbili ya mwezi marchi watu watano waliuawa na
wananchim kwa kuwatuhumu kuwa wanajihusisha na imani za kishirikina na tarehe
saba ya mwezi wa pili kijiji jirani cha lubanda waliuawa watu wawili na kuchoma
moto nyuma saba kwa kama tuhuma hizo hizo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MAITI YENYE UTATA YAFUKULIWA NA KUKUTWA IMEKATWA SEHEMU YA VIUNGO NA SEHEMU ZA SIRI.”
Post a Comment