Saturday, April 4, 2015

LIVERPOOL YAFIA EMIRATES, YAPIGWA 4-1


Alexies Sanchez wa Arsenal akiifungia timu yake bao.

Kiungo wa Arsenal, Hector Bellerin, akishangilia baada ya kufunga bao la kwanza.


Staa wa zamani wa Arsenal, Thierry Henry, akiwapungia mashabiki wa timu hiyo mkono kwenye mchezo kati ya timu hiyo na Liverpool uliopigwa kwenye Uwanja wa Emirates.


Washika bunduki wa London, Arsenal leo wameifanyia mauaji, Liverpool kwa kuicharaza mabao 4-1, katika mchezo wa Ligi Kuu England, uliopigwa kwenye Uwanja wa Emirates, jijini London.

Katika mchezo huo uliokuwa wa kasi ulishuhudiwa wenyeji Arsenal wakienda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 3-0. Kinda Hector Bellerin alianza kuipatia bao dakika ya 37, kabla ya Mesut Ozili kuongeza la pili dakika tatu baadaye, kisha Alexis Sanchez kuongeza la tatu dakika ya 45.

Liver walionekana kubadilika kipindi cha pili, hasa baada ya kuingia kwa Daniel Sturridge, ambaye mara kadhaa aliisumbua ngome ya Arsenal na walipata penalti katika dakika ya 76 iliyofungwa na Jordan Hernderson.

Olivier Giroud alipigilia msumari wa mwisho katika dakika ya 91 na kuifanya Arsenal ichekelee Sikukuu ya Pasaka.Ushindi huo umeifanya Arsenal kupaa hadi nafasi ya pili na pointi 63, mbili mbele ya Manchester City ambao watashuka dimbani Jumatatu.

 

0 Responses to “LIVERPOOL YAFIA EMIRATES, YAPIGWA 4-1”

Post a Comment

More to Read