Sunday, April 5, 2015

NYOSSO AREJEA UWANJANI BAADA YA KUMALIZA ADHABU ILIYOTOKANA NA KUMPAPASA MAKALIO MAGULI





BEKI kisiki wa Mbeya City fc, Juma Said Nyosso anarejea uwanjani baada ya kumaliza kutumikia adhabu yake ya kufungiwa mechi nane (8) za ligi kuu soka Tanzania bara.
Adhabu yake ilitokana na kitendo cha udhalilishaji alichomfanyia mshambuliaji wa Simba Elius Maguli baada ya kumpapasa makalio kwenye mechi ya ligi kuu iliyopigwa januari 28 mwaka huu uwanja wa Taifa, Dar es salaam, Mbeya City ikishinda 2-1.

Baada ya Gazeti la michezo la Champion kuanika picha mnato ikimuonesha Nyosso akimpapasa Makalio Maguli, TFF kupitia kamati zake za nidhamu ilitangaza adhabu ya kifungo cha mechi nane februari 6 mwaka huu baada ya mechi ya Mbeya City na Polisi Morogoro uwanja wa Jamburi, City ikilala 1-0.

Ili kuonesha uungwana, Nyosso alikiri kufanya kosa na kumuomba radhi Maguli.

Nyosso alianza kutumikia adhabu yake katika mechi ya Mbeya City dhidi ya JKT Ruvu uwanja wa Azam Complex februari 7 mwaka huu, timu hizo zikitoka sare ya 1-1.

Mechi amekaa nje ya uwanja kwa mechi 8 na sasa anarejea uwanjani kuwakabili Azam fc katika mechi ya ligi kuu itayopigwa jumatano, aprili 8 mwaka huu uwanja wa Azam Complex.

Kocha mkuu wa Mbeya City fc, Juma Mwambusi amefurahishwa na kurejea kwa beki wake huyo aliyekuwa na muunganiko mzuri na Yusuph Abdallah.


0 Responses to “NYOSSO AREJEA UWANJANI BAADA YA KUMALIZA ADHABU ILIYOTOKANA NA KUMPAPASA MAKALIO MAGULI”

Post a Comment

More to Read