Friday, June 27, 2014
27 Jun 2014 MKE WA MAREHEMU GEORGE TYSON ATINGA NYUMBANI KWA MAREHEMU NA KUDAI MALI ZAKE
Do you like this story?
Mke wa marehemu George Otieno ‘Tyson’, Beatrice Shayo. |
Mke wa Tyson (kulia) na ndugu zake wakisubili getini. |
Wakati hata siku arobaini hazijatimia,
mke wa marehemu George Otieno ‘Tyson’, Beatrice Shayo juzi alicharukia mali
zake baada ya kuamua kutinga nyumbani kwa marehemu, Mbezi Makonde jijini Dar
kwa lengo la kuchukua kila kinachomhusu.
Mdada huyo aliyefunga ndoa na Tyson
Agosti 9, 2012 nchini Kenya na kujaaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume aitwaye
Eugene, alishuhudiwa na gazeti hili Juni 24, mwaka huu saa sita usiku akiwa na
ndugu zake na kuanza kugonga geti la nyumba hiyo.
Katika kujua kilichokuwa kikiendelea,
mmoja wa mapaparazi wetu aliwasogelea na kuzungumza na Beatrice ambaye alieleza
kuwa, lengo lake lilikuwa ni kuchukua mali zake zilizomo mle ndani.
“Ulidhani mimi nataka kuingia kwenye nyumba hii nikae, la hasha! Nimefuata mali zangu tu basi,” alisema Beatrice huku akiendelea kugonga geti hilo.
Wakati Beatrice na nduguze wakionekana
kukata tamaa ya kufunguliwa, mara alitokea mwanamke anayedaiwa alikuwa akiishi
na marehemu mpaka kifo kilipomkuta na kuuliza aliyegonga geti ni nani,
alipotajiwa jina la Beatrice alisema: “Eee, Beatrice, usiku huu umekuja
kutafuta nini?”
Beatrice: Nina shida, naomba ufungue tuongee.
Beatrice: Nina shida, naomba ufungue tuongee.
Mwanamke: Hatuwezi kuongea usiku huu,
uje kesho asubuhi.
Beatrice: Nakuomba ufungue tu, nimekuja kuchukua mali zangu nilizoacha humo ndani na nimekuja na gari kabisa la kubebea.
Beatrice: Nakuomba ufungue tu, nimekuja kuchukua mali zangu nilizoacha humo ndani na nimekuja na gari kabisa la kubebea.
Mwanamke: Mali gani, humu hamna chako
na kama una kitu chako humu, fuata taratibu.
Beatrice: Nimefuata taratibu, nipo na mjumbe hapa.Mwanamke: Ndiyo nasema mje kesho asubuhi na mapema mtanikuta.
Baada ya mwanamke huyo kugoma kufungua, mjumbe wa eneo hilo aliyefahamika kwa jina la Sabina Mawanda aliwashauri waondoke na kurudi tena asubuhi lakini inadaiwa walipofanya hivyo walikuta nyumba imefungwa na hakukuwa na mtu.

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ 27 Jun 2014 MKE WA MAREHEMU GEORGE TYSON ATINGA NYUMBANI KWA MAREHEMU NA KUDAI MALI ZAKE”
Post a Comment