Saturday, November 1, 2014
AJINYOGA HADI KUFA AKIWA MCHEPUKONI MBEYA
Do you like this story?
![]() |
Njemba ikiwa
imekufa baada ya kujitia kitanzi ndani ya nyumba ya mchepuko eneo la mama John
Mbeya (Tunaomba radhi kwa picha hizi)( Picha David Nyembe Fahari news)
|
![]() |
Majirani wakilia kwa uchungu |
![]() |
Mke wa Marehemu akiwa chini baada ya kushudia mwli wa marehemu mumewe ambaye ameachwa na watoto watatu.. |
Na Mwandishi wetu,Mbeya
Katika hali isiyokuwa ya kawaida
Mkazi wa eneo la Mama John Mtaa wa Kagera jijini Mbeya ambaye jina lake
halijafahamika mara moja maarufu (Malebo) Dereva wa Daladala (34)
amekutwa amejinyonga hadi kufa ndani ya nyumba ya mpenzi wake (Mchepuko)
Octoba 31 mwaka huu .
Tukio hilo la aina yake limetokea
majira ya saa 7 jioni katika eneo la Mama John jijini hapa ambapo inadaiwa kuwa
chanzo cha tukio hilo ni wivu wa mapenzi kwani marehemu huyo ilikwenda
kwa mpenzi wake (Mchepuko)na kukuta nyumba ikiwa wazi bila kuwa na
dalili za kuwa na mtu ambapo mara baada ya kuuliza majira alielezwa kuwa
mwanamke huyo hakuonekana nyumbani hapo kwa usiku mzima nakwamba hakulala
kwakwe.
Aidha baada ya kupata majibu hayo
mwanaume huyo aliondoka na kwenda kwa marafiki zake sehemu wanayouzia pombe za kienyeji
maarufu (Vamponji) na kuomba ushauri juu ya nini afanye ili kukabiliana
na hali hiyo.
Alidaiwa kuwa mwanaume huyo
wakati akiomba ushauri alieleza kuwa mpenzi wake huyo ambaye alijulikana kwa
majina ya Rebeka Dankeli maarufu Mama Chausiku alihisi amekwenda kulala
kwa mwanaume mwingine kwani wamekuwa wakigombana kw amuda mrefu juu ya kuwepo
kwa hali hiyo.
Wakati akitoa malalamiko hayo kwa
marafiki zake alielezwa kuwa nivema mambo hayo wakayamaliza wenyewe kwani
imekuwa kero kwao hasa kutokana na kwamba wamekuwa wakigombana mara kwa mara na
kushulishwa na majirani hao hivyo wamechoka na kwamba aondoke na akayamalize
yeye mwenyewe.
Kutokana na hali hiyo mwanaume
huyo aliondoka katika eneo hilo la kuuzia pombe za kienyeji iliopokwenda kupata
ushauri na kurudi katika nyumba anapoishi hawala yake huyo huku akiendelea
kutafakari yale yanayomsibu katika moyo wake pamoja na kuangalia kama mwanamke
huyo atarudi au laa.
Baada ya kukaa kwa muda mrefu
pasipo kumona mpenzi wake ambapo ilikuwa imefika majira ya saa mbili kasoro
aliamua kuchukua maamuzi ya kukatisha uhai wake kwa kujinyonga.
Akizungumzia hali hiyo Mwenyekiti
wa Mtaa huo Ndugu Anyokisye Mwambona amesema tukio hilo la kujinyonga kwa
mwanaume huyo nilakwanza kutokea katika maeneo hayo.
Amesema taarifa za kujinyonga
alizipata majira ya saa mbili kasoro ambapo alichukua jukumu la kutoa taarifa
kwa jeshi la polisi kwa lengo kutoa mwili wa marehemu huyo ndani ya nyumba
hiyo.
Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo
anasema mwanaume huyo tayari alikuwa na mke wake na alikuwa na watoto watatu
hivyo tukio hilo limetokea kwa nyumba ndogo (Mchepuko) nakwamba kesi juu
ya mwanaume huyo amekuwa akizipata mara kwa mara hivyo hatua ya mwanaume
huyo kujinyonga inawezekana ikawa ni wivu wa mapenzi.
Amesema tuko hilo liliteka hisia
za wakazi wengi wa eneo hiloo kwani mwanaume huyo alikuwa na familia yake hivyo
maamuzi aliyoyachukua ni makubwa na yataigharimu familia yake kwa kiasi kikubwa
hasa kutokana na watoto wenye kuwa na umri mdogo pamoja na mke wake kutokuwa na
shughuli yoyote.
Vilio na majonzi yalitawala baada
ya mke wa marehemu huyo halali alipofika katika eneo hilo la tukio na kuanza
kulia kwa sauti kubwa huku akitamka maneno ambayo yaliwaliza wengi walitokea
katika tukio hilo.
Alidai kuwa amekuwa akimkanya
mumewe huyo kwa muda mrfu juu ya kuachana na mwanamke huyo lakini amekuwa
hasikii hivyo yaliyokumkuta ni ukaidi wake alieleza mama huyo huku akitazama
mwili wa mumewe ukuwa juu uneninginia .
Hata hiyo Kamanda wa polisi
Mkoani hapa Ndugu Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo
ambapo mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospital ya rufaa mbeya.
Mwisho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “AJINYOGA HADI KUFA AKIWA MCHEPUKONI MBEYA”
Post a Comment