Sunday, November 2, 2014
TUNAOMBA RADHI KWA PICHA_KITU KINACHODHANIWA KUWA BOMU CHAUA MTU MMOJA HUKO KISHAPU,MAJERUHI WATATU
Do you like this story?
Tarehe 01/11/2014 muda wa saa 07:45hrs
katika center ya Mhunze tarafa ya Kishapu na Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga
kumetokea kifo cha mtu mmoja na watu watatu kujeruhiwa na kitu kinachodhaniwa
kuwa ni bomu kulipuka ndani ya gari.
Gari hilo ni lenye namba za
usajili T. 848 AKA MITSHUBISH FUSSO likiendeshwa na Khalifa s/o Mussa 39,
muhangaza wa Ngara ambalo lilitoka tarehe 31/10/14 saa 04:00 hrs mjini Ngara
kuja Mkoa wa Shinyanga wilaya ya Kishapu kupakia shehena ya mtama kwa
mfanyabiashara alitwaye Donard s/o Nzugula (49) mkazi wa Muhunze.
Inaelezwa
kuwa wakati gari hilo likiwa limeegeshwa dukani kwa mfanyabiashara huyo ili
kusubiri kupakia mzigo huo dereva alishuka kununua sigara maduka ya jirani
akamwacha utingo wake ndani ya gari peke yake ambaye anaitwa Juma s/o Rashid
21-23, mkazi wa Ngara ambaye ni familia ya mwenye gari(aliyefariki dunia)
Baada ya muda mfupi kama dakika 15 hivi
dereva alisikia mshindo mkubwa na alipokwenda kwenye gari alimkuta utingo wake
ametupwa nje ya gari na akiwa amefariki mwili wake ukiwa na majeraha
tumboni,mkono wa kushoto kiganja kimekatika,mkuu wa kulia kwenye paja ambalo
limechimbika hadi kwenye mfupa, shingoni upande wa kushoto kuna shimo kubwa
lililosababishwa na kitu chenye ncha kali.
Pia mfanyabiashara Donard Nzugirwa Mwalimu ambaye ameumia mkono wa kulia kwa kuchanwa chanwa na vipande vya chuma,amepelekwa hospitali ya mkoa kwa matibabu zaidi.
Wengine ni Maganga Pius (14 ), mkazi wa Kishapu ambaye amejeruhiwa paja la kushoto,mgongoni na mkono wa kushoto.
Seni Edward (25 ), ambaye amejeruhiwa bega la kushoto, majeruhi
wote wametibiwa na kuruhusiwa.
Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na
kwamba linafanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha tukio hilo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ TUNAOMBA RADHI KWA PICHA_KITU KINACHODHANIWA KUWA BOMU CHAUA MTU MMOJA HUKO KISHAPU,MAJERUHI WATATU ”
Post a Comment