Sunday, November 2, 2014
JUMLA YA WASICHANA 6,000 MKOANI MTWARA WAPO KATIKA NAFASI NZURI YA KUJIKINGA NA MIMBA NA VIRUSI VYA UKIMWI
Do you like this story?
Jumla ya wasichana 6,000 mkoani Mtwara walio kwenye umri wa balehe sasa
wapo katika nafasi nzuri ya kujikinga na mimba za umri mdogo zinazowasababishia
kuacha shule pamoja na kujikinga na maambukizi ya Virusi vya
Ukimwi
Akiongea jijini Dar es Salaam jana, Meneja uhusiano na
mawasiliano wa T-MARC Tanzania Maurice Chirimi alisema mafanikio hayo
yametokana na mradi unaojulikiana kama ‘Hakuna Wasichoweza’ unaotekelezwa na
T-MARC kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) na Kampuni ya
mawasiliano ya Vodacom.
Chirimi alisema kuwa, mradi huo ulianza mwaka 2013 ambapo USAID kwa
kushirikiana na Vodacom kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii (Vodacom
Foundation waliwapa nguvu ili kufanikisha mradi huo.
Alifafanua kuwa, kupitia mradi huo, T-MARC imefanikisha kutoa mafunzo kwa
wasichana walio mashuleni na wasio mashuleni ikiwa na lenga la kuwapatia elimu
pamoja na kuwapatia pedi wasichana wanatoka katika familia maskini kwa ajili ya
kujihifadhi wakati wakiwa hedhi.
Aliongeza kuwa, mafunzo pamoja na pedi za bure zimewafikia wasichana
5,232 waliopo katika shule 24 za msingi na wengine 552 wasiokuwepo mashuleni
katika kata 17 mkoani Mtwara.
“Mafunzo ya namna na kujihifadhi wakati wakiwa hedhi pamoja na afya ya
uzazi yanafanyika chini ya uwezeshaji wa walimu waliopewa mafunzo na wauguzi wa
jadi. Kitini cha kufundishia juu ya masuala haya kimeweza kuandaliwa na T-MARC
kwa kushirikiana Taasisi ya Elimu Tanzania kupitia mradi huu wa ‘Hakuna
Wasichoweza’,” alifafanua
Alisema kupitia mafanikio yaliyopatikana kwenye awamu ya kwanza ya mradi,
T-MARC kwa msaada wa dola za Kimarekani 166,000 itaupanua mradi na kuwafikia
wasichana wengine 4,200 katika shule mpya 10 na kuongeza kuwa pia shirika lake
litawapatia mafunzo walimu wengine 20 kwa ajili ya kuwafundisha na kuwaelekeza
wasichana
Kwa upande wake, Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom
Rosalynn Mworia alisema Vodacom Foundation ikitambua mchango wa mwanamke katika
jamii inayomzunguka kwani ukimwelimisha mwanamke ni sawasawa na kuelimisha jamii,
Kwa kweli Vodacom foundation inajivunia sana kufadhili mradi huo muhimu.
Alisema mara nyingi ukosefu wa elimu sahihi juu ya
afya ya uzazi umekuwa ukiwafanya wasichana kuanza kuacha kuhudhuria vipindi
vyao mashuleni yote hayo pia ni kwa kukosa nguo za kujihifadhi wakiwa katika
siku za hedhi na kuwafanya watoto kuanza ngono wakiwa katika umri mdogo bila
kujua madhara yake jambo ambalo huwasababishia mimba na kuwafanya washindwe
kutimiza ndoto zao za kielimu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ JUMLA YA WASICHANA 6,000 MKOANI MTWARA WAPO KATIKA NAFASI NZURI YA KUJIKINGA NA MIMBA NA VIRUSI VYA UKIMWI ”
Post a Comment