Friday, November 7, 2014

WAZABUNI MBEYA KUISHTAKI SERIKALI.




Chama cha Wazabuni Mbeya (Chawambe), kinakusudia kuiburuza mahakamani serikali ya mkoa kwa madai ya kushindwa kuwalipa wanachama wake wenye zabuni ya kusambaza vyakula na vifaa vingine serikalini.

Mwenyekiti wa Chawambe, Yahya Lema alisema hilo jijini hapa jana na kuongeza kuwa, wamefikia hatua hiyo baada ya kutolipwa Sh1 bilioni wanazoidai kuanzia mwaka 2007 hadi sasa.

“Hali yetu ni mbaya, tumefilisika kabisa, kuna baadhi wamesitisha kusambaza vyakula... taasisi tunazozidai zimekuwa zikitupiga chenga kutulipa fedha zetu,” amesema.

Akizungumzia malalamiko hayo, Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja alisema hafahamu chochote kuhusiana na suala hilo.

Alisema ni vyema wazabuni hao wakampelekea orodha ya taasisi zinazodaiwa ili kuangalia tatizo liko wapi, kwa kuwa inawezekana fedha hizo zinatolewa na Serikali, lakini hazifikishwi sehemu husika.

Hata hivyo, Mtunguja alisema kuna halmashauri ambazo hupokea fedha kutoka serikalini kuwalipa wazabuni wake au fedha huingizwa benki moja kwa moja kutoka serikalini.

0 Responses to “WAZABUNI MBEYA KUISHTAKI SERIKALI.”

Post a Comment

More to Read