Friday, January 23, 2015
AJUZA MIAKA 90:ANASOMA DARASA LA NNE NCHINI KENYA.
Do you like this story?
Akiwa na umri wa miaka 90 mwanamke wa Kenya ambaye
anahudhuria masomo akiwa na wajukuu zake wapatao sita inaaminika ndiye
mwanafunzi mzee zaidi anayesoma shule ya msingi duniani.
Akiwa
ameketi dawati la mbele kabisa darasani ,yuko darasa la tano na amevalia nguo
za shule , Priscilla Gogo Sitienei anamsikiliza mwalimu anayefundisha kwa
makini hukua akiandika majina ya wanyama kwa kiingereza kwenye daftari lake.
Prissilla
alijiunga na shule hii ya Leaders Vision Preparatory School miaka mitano
iliyopita lakini pia aliwahi kuwahudumia wakaazi wa kijiji chake cha Ndalat
kilichoko kwenye bonde la ufa kama mkunga miaka sitini na mitano iliyopita.
Darasani
Priscilla anawasaidia wengine wafanye vyema ambao wana umri kati ya miaka 10
hadi 14 na mar azote huwaambia ujumbe wake hasa mabinti kuwa elimu ndiyo urithi
wao.
Priscilla
anajulikana kama Gogo maana yake bibi katika lugha ya jamii ya
wakalenjini,anasefurahia masomo akiwa na umri wa miaka 90 katika umri huo
anajua kuandika na kusoma pia fursa aliyoikosa alipokuwa mdogo.
Lugha
ambayo Priscilla anajiona yuko huru kuitumia ni lugha mama kwake ki Kalenjin
kuliko kiingereza,pindi anapotakiwa kujieleza kwanini aliamua kujiunga na shule
katika umri wake.
Sababu
kubwa ambayo amekuwa akiitoa,ni ajue kusoma ili amudu kusoma bibilia,lakini pia
kwa umri wake anataka awahamasishe watoto kupata elimu,kwani anawaona watoto
wengi wakiwa hawako shuleni na watoto hao wana watoto.
Gogo
apitapo mitaani haoni shida kukabiliana na watoto ambao hawako shuleni katika
muda wa masomo na kuwauliza kwanini hawako shuleni.
Gogo anasema
watoto hao humjibu kwamba hawaendi shule kwakuwa umri wao ni mkubwa,name
huwaambia mimi ni mkubwa sana kwenu lakini niko shuleni hivyo nanyi jiungeni na
shule.
Kikubwa
kinachomuumiza Gogo ni kuwaona watoto wengi waliopoteza muelekeo,wengi wao
hawana baba na wanazurura hovyo mitaani,bila msaada wowote.kutokana na hali
hiyo nataka kuwahamsisha waende shuleni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “AJUZA MIAKA 90:ANASOMA DARASA LA NNE NCHINI KENYA.”
Post a Comment