Tuesday, January 27, 2015
DHORUBA KUBWA YA THELUJI NA UPEPO MKALIKUPELEKEAKUSIMAMA KWA HUDUMA ZA UMMA KASKAZINI MASHARIKI YA MAREKANI
Do you like this story?
![]() |
Lori maalumu la usafishaji likiondoa theluji iliyoenea katika barabara ya South Church Street, katika mji wa Hazleton, Pennsylvania siku ya Jumatatu Jan 26, 2015. Photo via .dailymail.co.uk |
Zaidi ya watu
60 million wataathirika kutokana na kimbunga kikubwa cha upepo unaoambatana na
unyeshaji wa theleji katika eneo la kaskazini mashariki ya Marekani.
Kwa mujibu wa
kitengo cha hali ya hewa nchini Marekani, imetaja maeneo ambayo yataathiriwa na
dhoruba hiyo, ya kihistoria ambayo itapelekea zaidi ya watu kadhaa kukosa
huduma ya umeme, pamoja na huduma za usafiri wa anga na nchi kavu.
Imetaja
baadhi ya majimbo ambayo yatakumbwa na kimbunga hicho kuwa ni New York, New
Jersey, Massachusetts, Connecticut na Rhode Island, ambapo viongozi wakuu
wamajimbo hayo kutangaza hali ya hatari kwa tukio hilo ambalo litatokea siku ya
Jumatatu, Jumanne na Jumatano.
Imetabiriwa
kiasi cha unyeshaji wa theluji hiyo 36inches katika jimbo la New York 16 hadi
26 inches katika jimbo la Boston, na kiwango chengine kama hicho katika baadhi
ya majimbo mengine.
Zaidi ya
safari za ndege 3,800 zimesimamishwa mapema leo katika viwavya vya ndege vya
JFK, LaGuardia na Newark airports, pia huduma za shule kufungwa siku ya jumanne
na jumatano katika majimbo hayo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “DHORUBA KUBWA YA THELUJI NA UPEPO MKALIKUPELEKEAKUSIMAMA KWA HUDUMA ZA UMMA KASKAZINI MASHARIKI YA MAREKANI”
Post a Comment