Tuesday, January 27, 2015
RUNGU LA FAINI LAMWANGUKIA MNYAMA SIMBA.
Do you like this story?
Na
Bertha Lumala, Dar es Salaam
Klabu
ya Simba italimwa faini na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kutopeleka
timu uwanjani wakati wa mechi yao iliyopita dhidi ya Azam FC.
Simba
haikupeleka kikosi B kumenyana na kikosi B cha Azam FC kabla ya kuanza kwa
mechi yao ya raundi ya 12 ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam jana.
Humphrey
Nyasio, msemaji wa Simba, ameuambia mtandao huu jijini hapa kuwa wamefanya kosa
hilo kutokana na "matatizo ya ndani ya uongozi wa klabu."
"Hatukupeleka
timu yetu ya vijana uwanjani jana kwa sababu haikufanya mazoezi wiki iliyopita
kutokana na matatizo ya ndani ya uongozi ambayo sijapewa ruhusa ya
kuyazungumzia kwa sasa," Nyasio amesema na kuongeza:
"Kuna
kikao kinaendelea Rais (Evans Aveva) amekutana na Kamati ya Ufundi, Ninafikiri
kesho tutakutana na waandishi wa habari kuelezea kwa kina suala hilo."
Hata
hivyo, taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Simba, zinadai kuwa wachezaji wa
Simba B wamegoma kufanya mazoezi kutokana na kutolipwa posho.
Simba
itapigwa faini ya Sh. 500,000 na Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) kwa kutopeleka kikosi
B uwanjani, kwa mujibu wa Kanuni za Ligi za TFF toleo la 2014.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “RUNGU LA FAINI LAMWANGUKIA MNYAMA SIMBA.”
Post a Comment