Thursday, January 22, 2015
HIVI NDIVYO POLISI WALIVYOUAWA KATIKA TUKIO LA UMAVIZI KITUONI IKWIRIRI NA SILAHA KUIBWA NA MAJAMBAZI
Do you like this story?
![]() |
Kamishana wa Polisi Oparesheni na Mafunzo, Paulo Chagonja, katika picha hii ya maktaba akizungumzia tukio la uvamizi wa kituo cha Polisi Ushirombo. |
ASKARI wawili wa
Jeshi la Polisi katika Kituo cha Ikwiriri wilayani Rufiji mkoani Pwani,
wameuawa baada ya kushambuliwa kwa silaha na majambazi, waliovamia kituo hicho
na kuiba silaha baada ya kufanikisha mauaji.
Kutokana na tukio
hilo, Jeshi la Polisi liko katika msako mkali, huku Mkuu wa jeshi hilo, IGP,
Ernest Mangu akitangaza donge nono la Sh milioni 20 kwa watakaofanikisha
kukamatwa kwa wahusika wa tukio hilo na silaha.
Akizungumza na
waandishi wa habari kwa njia ya simu kutoka eneo la tukio, Ikwiriri, Kamanda wa
Polisi mkoani Pwani, Ulrich Matei alisema majambazi hao walitumia silaha kuwaua
askari hao.
Kamanda Matei alisema
kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 8 usiku katika kituo hicho cha Polisi
cha Ikwiriri.
Aliwataja askari
waliokufa kuwa ni mwenye namba E 8732 Koplo Edgar Milinga na WP 5558 Konstebo
Judith Timothy.
Alisema licha ya
kufanya mauaji hayo, pia majambazi hao yalipora silaha tano za moto aina
mbalimbali, zikiwemo SMG 2, SAR 3 na risasi 60. Pia, walichukua mabomu mawili
ya machozi.
Kamanda alisema kuwa
pia watu hao, waliharibu kwa kulipiga risasi gari la Polisi la kituo hicho
lenye namba za usajili PT 1965.
Msemaji wa Jeshi la
Polisi nchini, Advera Bulimba alisema tukio hilo la kusikitisha, halitapita
hivi hivi, bali jeshi limeelekeza nguvu zake huko kuhakikisha wahusika
wanakamatwa.
Alisema tayari Mkuu
wa Jeshi ametangaza dau la Sh milioni 20. Pia, alisema katika kuongeza kasi ya
msako, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo, Paul Chagonja akiwa na timu ya
makachero, yuko eneo la tukio kuhakikisha wahusika, kokote waliko, wanasakwa na
kutiwa mbaroni.
“Hili ni sawa na
tukio la kigaidi, Jeshi la Polisi litakabiliana na wahusika kokote waliko,
lazima wakamatwe.
Kikubwa tunaomba
ushirikiano wa wananchi, tunaamini wengi ni raia wema na watalisaidia jeshi
kufanikisha jukumu hilo la kukomesha uhalifu nchini,” alisema Advera.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “HIVI NDIVYO POLISI WALIVYOUAWA KATIKA TUKIO LA UMAVIZI KITUONI IKWIRIRI NA SILAHA KUIBWA NA MAJAMBAZI ”
Post a Comment