Thursday, January 22, 2015
WANAFUNZI 459 WA DARASA LA KWANZA WANASOMEA KWENYE DARASA MOJA JIJINI DAR
Do you like this story?
Katika hali isiyo ya
kawaida, zaidi ya wanafunzi 459 wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Saku
iliyopo Chamazi, Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, wanasoma katika
darasa moja.
Hali hiyo ya
wanafunzi kusoma katika darasa moja na wengine chini ya miti inayozunguka shule
hiyo, inachangiwa na upungufu wa majengo ya shule hiyo ambayo ina vyumba saba
vya madarasa huku ikiwa na zaidi ya wanafunzi 2,038.
Mwalimu Mkuu wa Shule
ya Msingi Saku, Salome Munisi alisema shule yake inakabiliwa na changamoto
kubwa ya uchache wa madarasa pamoja na wingi wa wanafunzi kuliko uwezo wa
vyumba vya madarasa walivyonavyo.
Munisi alisema idadi
ya wanafunzi walioandikishwa darasa la kwanza mwaka huu ni kubwa kuliko darasa
la pili ambalo lina wanafunzi 436, wakiwamo wanaume 217 na wasichana 219.
“Kipindi
cha mitihani inabidi wanafunzi wafanye mtihani chini ya mti kwa sababu wako
wengi darasani, huwezi mwalimu kuwapa mtihani watatizamiana na itakuwa ngumu
kupima kiwango cha elimu kwa wanafunzi kwa sababu watajaza majibu yote
yanayofanana“:- Munisi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WANAFUNZI 459 WA DARASA LA KWANZA WANASOMEA KWENYE DARASA MOJA JIJINI DAR ”
Post a Comment