Monday, January 19, 2015
MBEYA CITY FC SASA HAINA MASIHARA, YATUA DODOMA KUANDAA MAJESHI YA KUWAMALIZA WAJELAJELA.
Do you like this story?
WAGONGA
Nyundo wa Mbeya, Mbeya City fc leo jioni wanakabiliana na CDA ya Dodoma katika
mechi ya kirafiki itayofanyika uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma.
Afisa habari
wa Mbeya City, Dismas Ten ameuambia mtandao huu kuwa mechi hiyo ambayo ni
sehemu ya maandalizi ya mechi ya wikiendi dhidi ya mahasimu wao wa jiji,
Tanzania Prisons itatumiwa na kocha Juma Mwambusi kuongeza makali ya wachezaji
wake.
Kwa upande wa kocha mkuu Juma Mwambusi amekaririwa
na Tovuti ya klabu hiyo leo akisema: “Tumetoka kushinda mchezo
uliopita kwenye uwanja wa ccm kirumba na jumamosi ijayo tutakuwa na
mchezo mwingine huko Mbeya dhidi ya Tanzania Prisons, tuko hapa Dodoma kwa
maandalizi ya mchezo huo ingawa kwetu sisi kucheza na CDA ni sehemu ya
kudumisha udugu wetu kimichezo, binafsi nina imani kubwa na timu yangu na
kwa uwezo wa mwenyezi mungu naamini tutashinda pia mchezo
ujao wa ligi kwa sababu tunataka kupata pointi tatu kwenye kila mchezo
unaokuja mbele yetu”. Amesema Mwambusi.
Katika hatua nyingine Afisa masoko wa City Joseph
Semu amesema kuwa jezi za msimu huu zitakuwepo uwanjani hivyo mashabiki
wote wenye kiu ya kuvaa jezi hizo waje uwanjani na zitauzwa hapo kwa bei nzuri
kabisa.
Mbeya City
ilianza vibaya ligi, lakini safari hii imepata ushindi mara mbili mfululizo
kwani kabla ya kuifunga Kagera, iliitandika Ndanda fc bao 1-0 katika mechi ya ligi
kuu iliyopigwa desemba 28 mwaka jana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)


0 Responses to “MBEYA CITY FC SASA HAINA MASIHARA, YATUA DODOMA KUANDAA MAJESHI YA KUWAMALIZA WAJELAJELA.”
Post a Comment