Monday, January 19, 2015
JAJI MUTUNGI AVIONYA VYAMA VYA SIASA VINAVYOENDEKEZA MIGOGORO.
Do you like this story?
Hivi Karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la Migogoro ndani ya vyama vya
Siasa. Jambo hili linaleta Taswira mbaya kwa jamii, hasa kipindi hiki ukielekea
katika uchaguzi Mkuu wa nchi.
Athari za migogoro hii ni nyingi, ikiwemo chama cha kushindwa kutekeleza
majukumu yake kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa, kupoteza mvuto kwa jamii
na wanachama wake, ukosefu wa amani na utulivu ndani ya chama na kupoteza sifa
za usajili.
Hivi sasa mfumo wa demokrasi ya vyama vingi vya siasa una takribani miaka
23 tangu urejee tena mwaka 1992. Hivyo jamii inategemea kuwa mwanasiasa na
vyama vya siasa kuonyesha ukomavu na busara katika kuokuongoza na kushiriki
shughuli za chama.
Mojawapo ya ukomavu na ustarabu huo ni kuweka mifumo, kuongoza na
kushiriki shughuli za chama katika namna ambayo itaepusha migogoro.
Mojawapo ya Mambo ya kuzingatia ni chama kudhibiti tofauti za wanachama
na baina ya viongozi kwa njia ya kidemokasia na utawala bora katika kuongoza na
kushiriki shughuli za chama na kuheshimu na kufuata sheria, katiba na kanuni za
chama.
Hivyo natumia nafasi hii kama ninavyotambulika na jamii kuwa ni mlezi wa
vyama vya siasa, kuvisihivyama vyote vya siasa, kutekeleza wajibu wao kwa
mujibu wa sheria, katiba na kanuni zake. Pia kuwa mfano mzuri kwa jamii kwa
kudumisha amani na utulivu ndani ya vyama vya siasa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)



0 Responses to “JAJI MUTUNGI AVIONYA VYAMA VYA SIASA VINAVYOENDEKEZA MIGOGORO.”
Post a Comment