Monday, January 19, 2015
WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI WAFANYA FUJO, ASKARI WATUMIA NGUVU KUWATULIZA.
Do you like this story?
![]() |
| Wanafunzi wakivunja Geti |
Polisi nchinikenya katiika mji mkuu Nairobi leo imewafyetulia gesi ya
kutoa machozi wanafunzi wa shule ya msingi waliokuwa wakiandamana kupinga
unyakuzi wa ardhi waliyokuwa wanatumia kama kiwanja cha kuchezea na mmiliki
binafsi.
Polisi hao wakiwa na Mbwa waliwatawanyta wanafunzi hao, baadhi yao
wakisemekana kuwa watoto wenye umri wa miaka sita baada ya kuuangusha ukuta
mpya uliojengwa kati ya shule yao na uwanja huo.
Wanafunzi hao walikuwa wamerejea shuleni Lang'ata baada ya mgomo wa wiki
mbili wa walimu wa shule za umma walipopata kiwanja chao kikiwa kimeuzwa na
hata kuwekwa uzio.
Shule hio ina karibu watoto 1,000 walo kati ya umri wa miaka mitatu na
kumi na minne na inasimamiwa na baraza la jiji
Wanafunzi kadhaa walijeruhiwa katika purukushani hilo
wakati polisi walipoingilia kati na kujaribu kuwatawanya wanafunzi hao
waliokuwa wanazua rabsha.
Baadhi yao walipelekewa hospitalini baada ya kupata majeraha
madogomadogo.
Baadhi ya wanafunzi hao walikabiliana na polisi wakiwa wamebeba vijiti na
kuwanyoshea.
Polisi mmoja alijeruhiwa baada ya kupigwa kwa mawe.
Walimu wa shule hio pia waliandamana wakisaidiwa na wanaharakati wa
kisiasa.
Haijajulikana ambavyo mtu huyo aliweka uzio katika kiwanja hicho
walichokuwa wakitumia wanafunzi kuchezea.
Baraza la jiji limesema kuwa ardhi hio ni ardhi ya serikali ingawa
halijazungumzia ambavyo ardhi yenyewe iliuzwa ingawa wanaharakati wanasema
kiwanja hicho kimeuzwa kwa tajiri anayepanga kukitumia kwa ujenzi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)




0 Responses to “WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI WAFANYA FUJO, ASKARI WATUMIA NGUVU KUWATULIZA.”
Post a Comment