Tuesday, January 20, 2015
UCHAGUZI WA ZAMBIA KUFANYIKA LEO.
Do you like this story?
Hatimaye leo
wananchi wa Zambia wanapiga kura kuchagua Rais wa nchi hiyo, kufuatia kifo cha
Rais wa nchi hiyo Michael Sata Oktoba mwaka jana.
Chama tawala cha Patrioyoc Front kinauhakika wa
kushinda katika uchaguzi huo licha ya kukabiliwa na upinzani mkali kutoka
upinzani.
Waangalizi wa kikanda katika uchaguzi huo, wanasema
wameridhishwa na maandalizi ya zoezi zima la upigaji kura.Uchaguzi huo
unatarajiwa kuwa na upinzani mkali kati ya Edgar Lungu anayegombea nafasi hiyo
kupitia chama tawala na mpinzani wake HAKAINDE Hichilema kutoka United Party
for National Development.
Wagombea wote katika nafasi hiyo ya Urais wakati
wakijinadi wameahidi kuimarisha mfumo wa elimu nchini humo, kutengeneza ajira.
Huku wapiga kura nao wakitumaini kuwa wanasiasa hao watatimiza ahadi zao.Ikiwa
ni miaka 50 toka nchi hiyo ilipojipatia uhuru, Zambia imekuwa imara na
imeendelea na msimamo wake wa kufanya uchaguzi tangu kumalizika kwa siasa za
chama kimoja nchini humo.
Hata hivyo mshindi katika uchaguzi huo wa leo atatumikia
kipindi cha miezi 18 iliyobakia, katika awamu iliyobaki, aliyoiacha marehemu
Michael Sata, wakati nchi hiyo ikijiandaa kufanya uchaguzi mkuu mwakani 2016.
Vituo vya kupigia kura vitafunguliwa kuanzia saa 12
kamili asubuhi na kufungwa saa 12 jioni. Tume ya Uchaguzi nchini Zambia imesema
zoezi la uhesabuji kura, linatarajiwa kuanza muda mfupi tu baada ya zoezi la
upigaji kura kukamilika, huku matokeo yakitarajiwa kutangazwa katika kipindi
cha saa 48.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)


0 Responses to “UCHAGUZI WA ZAMBIA KUFANYIKA LEO.”
Post a Comment