Tuesday, January 13, 2015
NAFAHAMU TATIZO LA MISHAHARA YA POLISI: IGP MANGU.
Do you like this story?
Dar es Salaam. Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP),
Ernest Mangu amesema anatambua suala la kutobadilishwa mishahara ya
baadhi ya watumishi wake na kwamba, jambo hilo ni miongoni mwa ajenda
anazozifanyia kazi kwa sasa.
IGP Mangu alitoa ufafanuzi huo jana wakati
akizungumza na gazeti hili baada ya kuwapo malalamiko kutoka kwa baadhi
ya askari wa jeshi hilo kupandishwa vyeo, huku mishahara yao ikiendelea
kubaki kama ilivyokuwa zamani.
“Nimezunguka nchi nzima na kuzungumza na askari kuhusu jambo hili,” alisema Mangu.
Katika taarifa ambazo gazeti hili ilizipata, kuna
baadhi ya askari wamepandishwa vyeo na kudumu navyo hadi miaka miwili
sasa, lakini bila kurekebishiwa viwango vya mishahara.
Mmoja wa askari aliyezungumza na gazeti hili (jina
linahifadhiwa) alisema: “Nimepandishwa cheo miaka miwili sasa, lakini
jambo la kushangaza hadi leo mshahara wangu haujarekebishwa. Kwa namna
moja au nyingine, suala hili lina athari kwani unaonekana una cheo
kikubwa, lakini kiuchumi bado uko vilevile.”
Wengi wa askari wenye matatizo hayo ni wale
waliopandishwa kutoka NCO (askari wasio na kamisheni) na kupewa
kamisheni (Inspekta Msaidizi wa Polisi), ambao masilahi yao hutofautiana
ili kukidhi hadhi za vyeo hivyo.
IGP Mangu alifafanua kwa kusema: “Askari wote
wanajua kinachoendelea, kama kuna mwenye dukuduku lolote utaratibu wa
kupata taarifa upo wazi ndani ya jeshi.”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “NAFAHAMU TATIZO LA MISHAHARA YA POLISI: IGP MANGU.”
Post a Comment