Thursday, January 29, 2015

WAFANYABIASHARA JIJI LA MBEYA WAFUNGA MADUKA KWA KUPINGA KODI.


Maduka yakiwa yamefungwa



Wafanyabiasha katika jiji la Mbeya wakiwa katika Mkutano wa kujadili kupanda kwa Kodi.
Kaimu Meneja wa Tra Mkoa  Bw Anniny Lema  akijibu kero za wafanyabiashara kuhusiana na kupanda kwa kodi.



Mmoja wa wafanyabiashara akitoa kero zake mbele ya Viongozi wa Tra katika Ukumbi wa Mkapa Jijini Mbeya.



(Picha na Fahari News)           
Wakazi wa jiji la Mbeya wamekumbwa na adha ya kukosa huduma kwa ajili ya mahitaji mbalimbali  baada ya  wafanyabiashara  kufunga masoko na  maduka yao yote, kwa ajili ya kushiriki mkutano waliouitisha kwa ajili ya kujadili kodi ya TRA  inayodaiwa kuongezeka kwa asilimia 100.

Wafanyabiashara wa masoko na Maduka jiji la Mbeya jana walikubalina kusitisha kufanya biashara kwa siku nzima kwa ajili ya kushiriki katika mkutano huo  ulioshirikisha zaidi ya wafanyabishara 1000  uliofanyika katika ukumbi wa Benjamin Mkapa jijini hapa.

Wakuzingumza kwa nyakati tofauti  baadhi ya wakazi wa jiji la Mbeya walisema kuwa hali ni mbaya kutokana na kukosa  huduma  kwa ajili ya mahitaji ya kila siku hasa bidhaa za vyakula.

“Kwa leo hali ni mbaya hakuna biashara yoyote  chakula inayofanyika maduka  na masoko yamefungwa,mara baada ya kuuliza  wanatueleza kuwa wafanyabiashara wako kwenye mkutano hivyo familia zetu zimeathirika kwani  baadhi yetu hatuwezi kupata chakula kwa siku ya leo”alisema
Naye Joel Mwakyoma mfanyabiashara kutoka Makongorosi Wilayani Chunya alisema kuwa amesikitrishwa na hali aliyoikuta katika soko la sido kwani ndiyo soko analolitegemea kwa ajili ya kununua bidhaa za jumla kwa ajilli ya kwenda kuuza Chunya.

“Nimefika mapema leo  saa 2:00 kutoka Chunya kwa ajili ya kuja hapa soko la sido kwa ajili ya kujumua mahitaji ya duka langu lakini nimekuta soko na maduka yote yamefungwa hivyo natakiwa kurudi chunya au kulala hapa hadi kesho kitu ambacho ni hasara kwa biashara yangu”alisema

Mwakyoma ameishauri Serikali kupitia mamlaka ya mapato Tanzania (TRA)kumaliza mgogoro baina yake na wafanyabiashara ili kuweza kuondoa adha na migongano isiyo ya lazima ili kunusuru uvunjifu wa amani ambao unaweza kutokea hapo baadae.
Mwisho.

0 Responses to “WAFANYABIASHARA JIJI LA MBEYA WAFUNGA MADUKA KWA KUPINGA KODI.”

Post a Comment

More to Read